January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waajiri watakiwa kuweka mazingira bora ya kazi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

WAAJIRI wametakiwa kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa wafanyakazi ili wapate haki zao na kuhakikisha zinaweka mazingira mazuri
ya kufanyakazi wafanyakazi.

Hatua hiyo itawafanya wahamiaji wanapotoka kwenye nchi moja kwenda
katika nchi nyingine wakute mazingira mazuri na rafiki ya kazi.

Maelekezo hayo yametolewa jana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA ) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi Afrika Mashariki, (TUGHE) Hery Mkunda,
wakati wa kikao cha mtandao wa wafanyakazi wahamiaji wa Afrika unaofanyika chini ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi la Kimataifa.

Mkunda alisema kikao hicho ambacho zaidi ya washiriki 40 kutoka nchi za
Afrika Mashariki walishiriki, walijadili namna ya kuweka mfumo rafiki ambao utaakisi wafanyakazi wanalindwa na
kupata haki zao.

“Sisi kama wafanyakazi kupitia shirikisho la wafanyakazi Afrika tumeona ni muda muafaka kuungana wote kwa pamoja kushirikiana kuona jinsi gani tunaweka
mazingira katika nchi zetu kuhakikisha tunawalinda hawa wafanyakazi wanapata
haki zao, wanalindwa na kuhakikisha kwenye ajira zao wanapata haki za msingi”

“Wafanyakazi wahamiaji ili waweze kupata haki zao za msingi lazima wanapotoka
nchini Tanzania kwenda nchi nyingine lazima wawe salama na kulindwa,, alisema”

Mkunda aliipongeza Serikali kwa kuingia mkataba na nchi za Uarabuni ambao
utawasaidia wafanyakazi wanaotoka Tanzania kwenda nchi za Uarabuni na wao
wa Uarabuni kuja nchini Tanzania kuja kufanya kazi zao.