January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waajiri nchini watakiwa kuhakikisha wanasimamia sheria za afya na usalama makazini

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

WAKALA wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi OSHA wamewataka waajiri nchini kuhakikisha wanasimamia sheria za afya na usalama makazini ili kuweza kubaini madhara yanayoweza kuwapata watumishi wao makazini wakati wakitekeleza majukumu yao huku akiwataka
Wamiliki wa Viwanda na Taasisi Mbalimbali zinazoajiri Wafanyakazi kuendelea kufuata Sheria za OSHA katika Utekelezaji wa majukumu yao kwa Wafanyakazi.

Akizungumza mara baada ya kuwapatia mafunzo ya siku nne wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali jijini Tanga Erick Mororo ambaye ni ofisa mafunzo kutoka Osha makao makuu amesema kuwa lengo la kuwajengea uelewa juu ya usalama wao wakiwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ni jambo la muhimu hususani katika usalama wa afya zao.

Erick amewataka waajiri kuhakikisha maeneo yao yanakaguliwa kwa mujibu wa sheria lakini pia na watumishi wao wafanyiwe vipimo vya afya ili kuweza kubaini madhara yanayoweza kuwapata mahali pa kazi wakati wakitekeleza majukumu yao.

Aidha aliwataka Wamiliki wa Viwanda na Taasisi Mbalimbali zinazoajiri Wafanyakazi kuendelea kufuata Sheria za OSHA katika Utekelezaji wa majukumu yao kwa Wafanyakazi,

” Naendelea kuwahimiza Wamiliki wa Taasisi Mbalimbali zinazoajiri Wafanyakazi kuendelea kufuata Sheria za OSHA ili Wafanyakazi wao waweza kuwa Salama tutaendelea kufanya ukaguzi kuona Kama Sheria zetu zinafuatwa” Alisisitiza Erick.

Sambaba na hayyo Ofisa huyo alizitaja aina za Usalama ambazo Wafanyakazi wanatakiwa kuzifuata pindi wawapo makazini mwao.

“Mafunzo haya yamegawanyika katika Makundi mawili ambayo yakwanza ni Afya , Tunapozungumzia Afya hapa tunamaanisha mtu akiwa kazini hatakiwi kupata magonjwa yanayotokana na kazi yake mfano Madaktari ,manesi na Sasa hivi Kuna ugonjwa wa Corona wanapaswa wajue namna ya kujikinga, “alisema Erick.

Baadhi ya wawakilishi katika mafunzo hayo akiwemo Rashid Millian kutoka kampuni ya Maweni lime Stone na Angela Mlangwa kutoka kampuni ya Mohamed Interprises wamesena mafunzo waliyoyapata yatawasaidia kujikinga na vihatarishi mbalimbali pindi wawapo makazini.

Wamiliki wa Taasisi Mbalimbali zinazoajiri Wafanyakazi wameendelea kuhimizwa kufuata Sheria za OSHA ili Wafanyakazi wao waweza kuwa Salama mahala pa kazi ambapo zaidi ya Wafanyakazi 40 wanaendelea kupatiwa Mafunzo hayo ya siku nne jijini Tanga.