June 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vyombo vya habari vyatakiwa kuzingatia weledi kuelekea uchaguzi mkuu

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amevitaka vyombo vya habari nchini, hususani vinavyomilikiwa na chama hicho kuzingatia weledi, hasa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Akizungumza Juni 5, 2025, kwenye ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao na baadhi ya wakuu wa idara wa vyombo vya habari vya CCM, Balozi Nchimbi amesisitiza kuwa, weledi wa vyombo hivyo uendelee kuwa mfano wa kuigwa katika tasnia ya habari nchini.

Pia amesema vyombo hivyo ni sauti ya chama, vina jukumu la kuutangazia umma utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati chini ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020–2025,kuanza kuchambua Ilani mpya ya chama hicho kwa mwaka 2025–2030.

Huki akivisisitiza vyombo vingine vya habati nchini kufanya hivyo na kusema kuwa ni haki ya wananchi kupata taarifa mbalimbali zinazohusu maendeleo ya nchini yao.

Kwa upande wao, wawakilishi wa vyombo hivyo walieleza namna walivyojipanga kufikisha taarifa kwa jamii, zikiwemo elimu ya uraia kuelekea uchaguzi, namna ya kushiriki na mchakato wa kuwapata wagombea bora.