Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam.
KAMPUNI ya mtandao wa simu za mkononi Vodacom kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo benki ya Mwanga Hakika, imetenga kiasi cha bilioni 40 zitakazo tumika katika uendeshaji wa huduma mpya za mikopo kwa wateja wake zaidi ya milioni 19.
Akizungumza na Waandishi wa Habari,jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni ya ‘Maisha ni Kujiongeza na M-Pesa, Mkurugenzi wa Masoko na Biashara wa Vodacom, Linda Riwa,amesema kampuni hiyo kwa kushirikiana na tasisi hizo za kifedha, wameona ni vyema wakatambua mchango kwa wateja wao.
Ambapo wameamua kuja na kampeni hiyo ambayo itawezesha watumiaji wote wa mtandao wa Vodacoma kuweza kukopa mikopo mbalimbali ikiwa pamoja na mkopo mpya wa mafuta uliotambulishwa kama (Chomoka).
Mkopo wa akiba kwa wateja wa M-Pesa ( Mgodi),mkopo kwa wafanyabiashara,mkopo wa Mawakala (Wakala Songesha),mkopo kwa wateja binafsi pamoja na mkopo wa simu janja ( Smartphone).
Linda amesema, mikopo hiyo yote ni mipya ambayo imewekwa kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi wananchi wote hususani watumiaji wa mtandao huo huku akieleza kuwa mkopo wa chomoka una muwezesha mtumiaji wa chombo cha moto pindi anapokuwa hana pesa, kuweza kujaza mafuta bure katika kituo cha mafuta chochote chenye huduma ya lipa kwa M-Pesa na kulipa ndani ya siku 30.
“Kwakutambua mchango wa wateja wetu, tumetenga kiasi cha bilioni 40 kwa ajili ya kuendesha huduma zote hizi mpya ambazo tumezitambulisha leo, lengo ni kuwawezesha wateja wetu kuishi kidigitali,mtumiaji wa chombo cha moto pindi anapokuwa hana ‘cash’ anaweza kwenda kwenye sheli yoyote yenye huduma ya lipa kwa M-Pesa na atawekewa mafuta bure na atalipa ndani ya siku 30,”mesema Linda na kuongeza kuwa
“Kwa mawakala wote wa Vodacom, kuanzia sasa hakutakuwa tena na shida ya kuishiwa frot..kwani wakala pindi anapoona ameishiwa anauwezo wa kusongesha, ambapo atapata mkopo wa bila riba na huduma zake hazitasimama tena,”.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Biashara benki yac Mwanga Hakika, Projest Massawe, amesema kutokana na uhitaji wa Watanzania wengi kuwa na tatizo la kiuchumi kwa kushirikiana na Vodacoma wameona ni vyema wakatoa huduma hizo.
“Sisi Mwanga Hakika benki kwa kushirikiana na Vodacom tutahakikisha tunatoa huduma nzuri kwa wateja wetu wote, kwa Wakala pia ataweza kupata mkopo hadi wa milioni 10 ambazo atalipa ndani ya siku 30,”amesema Massawe.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu