Na Mwandishi wetu, timesmajira
WAWEKEZAJI wa Kampuni ya Elsewedy Electric kutoka nchini misri , imezindua rasmi uwekezaji wenye thamani ya zaidi ya dola za marekani milioni 400 wa kongani ya viwanda 100 vinavyotarajiwa kujengwa eneo la Mlandizi,Pwani.
Akizungumza katika uzinduzi wa uwekezaji huo uliofanyika mjini Cairo juzi ambapo ilienda sambamba na mkutano wa kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Misri,Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda wa Kampuni hiyo, Mohamed Alkaammah alisema uwekezaji wa kongani ya viwanda 100 ya kampuni hiyo inatarajia kuzalisha ajira zaidi ya 50,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
Amesema uwekezaji huo ni matunda ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoifaya nchini Misri mwaka 2021 ambapo aliwahamasisha wawekezaji hao kuja kuwekeza nchini.
”Tumeendelea kuwekeza nchini Tanzania kwa sababu ya uwepo was sera nzuri ya uwekezaji pamoja na ushirikiano uliopo unaotolewa na Serikali pamoja na kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania kuonyesha ushirikiano mkubwa kwetu,”amesema.
AmesemaTanzania kuna fursa nyingi ambapo wao wamewekaza wameweza kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa serikali hiyo inaonyesha ni kiasi gani biashara yao ni nzuri.
“Tunahaidi kushirikiana na Tanzania kuendelea kuwekeza na kufanya biashara na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha viwanda Afrika,”amesisitiza.
Kwa Upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji Nchini Tanzania,Gilead Teri amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuendelea kushirikiana na wawekezaji kutoka nchini Misri katika kuwekeza kwenye sekta mbalimbali.
Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara ambapo soko na uwekezaji wake unakuwa kwa kasi kutokana muingiliano wa watu mbalimbali
“Tupo katika jumuiya ya Afrika Mashariki na Sadc tunajumla ya uhakika la soko la watu takribani 450 ambapo kwa upande wa miundombinu iliyopo nchini Tanzania ni ya uhakika ikiwemo reli pamoja na barabara,”amesema.
Naye Rais wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Huru (GAFI) wa nchini Misri,Hassan Heiba amesema kuwa uhusiano wa kiuwekezaji baina ya Misri na Tanzania umekuwa mfano wa kuigwa wa ushirikano wa nchi za Afrika kwenye suala zima la uwekezaji.
Amesema kama nchi za Afrika zinatakiwa kushirikiana kwa pamoja kukuza uchumi wa nchi zao kwa kufanya uwekezaji wa pamoja miongoni mwa nchi zao kwa kushirikiana na nchi nyingine.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Elsewedy Electric Afrika Mashariki, Ibrahim Oamar amesema kuwa katika uwekezaji wao ambao tayari wameshafanya nchini Tanzania ikiwemo kuwa miongoni mwa kampuni zinazojenga bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere na kiwanda cha uzalishaji wa vifaa vya umeme vya (cables, wires and Transformers) umekuwa na mafanikio makubwa hasa kwa kupata soko katika nchi za Afrika mashariki na SADC.
“Tanzania ni miongoni mwa nchi yenye uchumi na utulivu wa kisiasa barani afrika na baada ya kupata manufaa ya uwekezaji tuliofanya ndo maana tumechukua hatua kubwa ya kuwekeza kwenye kongani ya viwanda,”amesema.
Kongani ya viwanda 100 ya ELSEWEDY ELETRIC INDUSTRIAL COMPLEX ni miongoni mwa uwekezaji wa kimkakati ambao pia utatumia bandari kavu ya kwala Pamoja na reli ya kisasa ya SGR kwa ajili ya kubebea mizig
More Stories
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?
Watendaji Songwe wapatiwa mafunzo uboreshaji daftari la mpiga kura
Samia: Mwaka 2024 ulikuwa wa mafanikio