May 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vivuko vipya suluhisho la usafiri Kanda ya Ziwa

Judith Ferdinand na Seleiman Abeid,Mwanza

Serikali baada ya kusikia kilio cha wananchi juu ya usafiri wa majini,iliwekeza kiasi cha bilioni 18.6 kwa ajili ya ujenzi wa vivuko vipya vitano huku vingine vikikarabatiwa.

Ambapo vivuko hivyo vinaelezwa kuwa suluhisho na utatuzi wa changamoto ya usafiri wa abiriia na mizigo kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa.

Hayo yamebainishwa na katika Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye ni Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa, baada ya kukagua ujenzi wa vivuko hivyo katika karakana ya kampuni ya Songoro Marine Transport  (SMT).Ikiwa ni ziara yake na waandishi wa habari wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga ya kumtembelea miradi ya maendeleo.

“Kazi imefanyika , halafu wanakuja watu wanasema hakuna kitu kilichofanywa na serikali,mbali na ujenzi wa vivuko hivi unaotekelezea na TEMESA,miradi mingine inafanyika Ziwa Taganyika na  katika Ziwa Nyasa chini ya TASHICO,”amesema Msigwa.

Mkurugenzi wa Uendeshaji  na Ujenzi wa Vivuko TEMESA, Mhandisi Masoud King’ombe,amesema miradi ya ujenzi wa vivuko vipya umefikia asilimia zaidi ya 90 pia kuna mradi wa ukarabati wa vivuko,huku vikitarajiwa kukamilika Septemba 2025 na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Ametaja vikuko vipya ni MV Bukondo kitakachotoa huduma kati ya Bwiro-Bukondo wilayani Ukerewe, MV Ijinga (Ijinga-Kahangara)wilayani Magu,MV Kome III kitahudumia Wilaya ya Sengerema kati ya Kisiwa cha Kome na Nyakaliro.

Pia MV Mbarika kitatoa huduma kwa wananchi wa Buyagu Sengerema na Mbarika, Misungwi huku MV Ukerewe kikiongeza nguvu ya utoaji huduma kati Rugezi Ukerewe na Kisorya Bunda.


Naye Mkurugenzi wa Songoro Marine, Major Songoro aliipongeza serikali kwa kuiamini kampuni hiyo ya kizalendo, kuteleza miradi inayolenga kutoa huduma  ya usafiri wa wananchi waishio pembezoni na visiwa vilivyopo ndani ya Ziwa Victoria.

“Tumejipanga kuhakikisha vinakamilika kwa wakati vikatoe huduma kwa wananchi,”amesema Songoro.