June 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vivo Energy Tanzania, yazindua Kampeni ya “Uliza Oili ya Shell”

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM

KAMPUNI ya Vivo Energy Tanzania imezindua rasmi kampeni yake mpya ya “Uliza Oili ya Shell” inalenga kuwaelimisha madereva, waendesha bodaboda, mafundi na wasafirishaji juu ya matumizi sahihi ya vilainishi, ikichochea ulinzi bora wa injini, kupunguza gharama za matengenezo, na kuongeza ufanisi wa matumizi ya mafuta.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Vivo Energy Tanzania Mohamed Bougriba amesema uzinduzi wa kampeni ya ‘Uliza Oili ya Shell,’ ni hatua muhimu inayolenga kutoa elimu sahihi kwa madereva na mafundi kuhusu vilainishi bora vya injini Kupitia teknolojia ya kimataifa ya Shell, tunaleta suluhisho halisi zinazolinda injini, kuongeza ufanisi wa mafuta, na kutoa thamani kwa watumiaji wetu.

Bougriba ameongeza kwa kushukuru wateja walioufanya mfululizo chapa ya Shell kuwa namba moja duniani kwa miaka 18, pamoja na kutangaza ushirikiano mpya wa kimkakati na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA).

“Tumeingia katika ushirikiano wa kimkakati na VETA ili kuwapatia vijana wa Kitanzania ujuzi muhimu katika huduma za vilainishi. Ushirikiano huu unafungua fursa za ajira na ujasiriamali kwa vijana wa Kitanzania.”

Kwa upande wake, Dkt. Aileen Meena, Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Miradi ya Jamii wa Vivo Energy Tanzania, amesema Kampeni ya ‘Uliza Oili ya Shell’ ni mwendelezo wa mafanikio ya kampeni ya mwaka jana ‘Sheli Tumerudi Kivingine.’ Tunalenga kubadili tabia, kuboresha huduma kwa injini, na kuchangia maisha bora kwa jamii kupitia elimu na uendelezaji wa ujuzi.

Kampeni hii inaleta pamoja bidhaa tatu kuu za vilainishi vya Shell ikiwemo Shell Advance – kwa pikipiki, bodaboda na bajaji: hutoa ulinzi wa kipekee wa injini, Shell Helix – kwa magari ya petroli: hutoa nguvu zaidi na kupunguza uchakavu, Shell Rimula – kwa magari ya dizeli kama malori na mabasi: hutoa ulinzi wa injini kwa safari za uhakika.

Naye Mratibu wa Kozi Fupi na Uzalishaji kutoka VETA, Mdillah Osward amepongeza Vivo Energy kwa utekelezaji wa haraka wa Mkataba wa Makubaliano, ambao ni ushirikiano wa kweli na wa vitendo, Mafunzo ya vitendo yanayotolewa yanawaandaa vijana kukabiliana na soko la ajira la sasa.

“Kwa ujumla, kupitia kampeni ya “Uliza Oili ya Shell,” Vivo Energy Tanzania inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama kampuni ya nishati yenye maono, inayowekeza katika watu, teknolojia, na jamii kwa maendeleo endelevu ya taifa”.