Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu(TPHPA) kumekuwa na vikwazo katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa mimea nchini kutokana na udanganyifu wa baadhi ya wauzaji wa viuatilifu.
Hali hiyo ni kutokana na uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu pamoja na kuwepo kwa wauzaji wa viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu na kusababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea.
Hayo yameelezwa a jijini hapa leo Machi 1,2023 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu (TPHPA) Dkt. Joseph Ndunguru wakati akieleze mafanikio na utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.
Dkt.Ndunguru amesema Mamlaka imeendelea kufanya kaguzi za biashara ya Viuatilifu ili kupunguza uwepo wa viuatilifu bandia ambapo jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji 198 vimesajiiliwa.
“Katika mwaka wa fedha 2022/23, Mamlaka imefanya uchambuzi wa sampuli 1,025 za viuatilifu ambapo sampuli 1,005 sawa na 98.04% zilikidhi viwango na sampuli 20 sawa na 1.96 % hazikukidhi,
“Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo, imefanya uchambuzi wa sampuli za udongo takribani 1,300 kutoka kwenye mashamba ya “Block farming” ili kuwezesha biashara ya mazao, sampuli 40 zilifanyiwa uchambuzi kwenye mazao mbalimbali na sampuli zote zilikidhi viwango na biashara ya mazao ilifanyika.
Aidha Dkt.Ndunguru, ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima atalazimika kutumia viuatilifu vingi ambapo itaathiri afya yake na mazingira kwa ujumla.
“Madhara ni mengi ndio maana tulitilia mkazo kwa kuwajengea uelewe wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu sababu wanapopulizia viuatilifu visivyosahihi vinawajengea usugu wadudu waharibifu na kuuwa wadudu rafiki wa mimea,”Dkt.Ndunguru
More Stories
Haya hapa matokeo yote kabisa ya Form Four
Kisarawe kukata keki Birthday ya Rais Samia
Mgeja aimwagia sifa CCM uteuzi wa Rais Samia, Mwinyi Urais 2025