Fresha Kinasa TimesMajiraOnline,Mara.
KATIKA kuhakikisha Wananchi wanafanya shughuli za maendeleo na kuzalisha vipato vyao vinavyochangiwa na Nishati ya umeme Katika Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara, serikali imeendelea na miradi ya kuviunganishia nishati hiyo Vitongoji vilivyopo jimboni humo.
Kazi zilizokamilishwa ni pamoja na Vijiji vyote 68 vimeunganishiwa umeme, yaani miundombinu ya usambazaji wa umeme imewekwa kwenye kila kijiji cha Jimboni humo.Hiyo ni sawa na asilimia 100 (100%) kwa upande wa vijiji vya Jimbo hilo.
Hayo yamebainishwa kupitia Taarifa ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini iliyotolewa Februari 21, 2025 ambapo imeeleza kuwa, Vitongoji 274, Kati ya Vitongoji 374 vya Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara vimeunganishiwa umeme,ikiwa ni sawa na asilimia 73.26 ya vitongoji vyote jimboni humo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa,”Kazi zinazoendelea kwa sasa (Bajeti 2024/25), na muda wa kukamilishwa kwake. Mkandarasi I: Vitongoji 59 +10
Mradi utakamilika kabla ya tarehe 16 Novemba 2025. Mkandarasi II: Vitongoji 15 Mradi utakamilika ndani ya mwaka huu, 2025.”imeeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa.
“Vitongoji 100 vilivyosalia.
Bajeti ya 2025/26 inayotayarishwa
Vitongoji 50 vitaunganishiwa umeme. Na Vitongoji 50 vinavyosalia, Uunganishwaji wa umeme kwenye hivyo vitongoji 50 utakamilishwa kwa kutumia Bajeti ya Mwaka 2026/27 au kwa kutumia fedha zitakazopatikana kabla ya Bajeti ya 2025/26 kukamilika. Ambapo taarifa hiyo ni kutoka REA kwenda kwa Mbunge wa Jimbo.”imeeleza taarifa hiyo.
Kwa upande wao Wananchi Jimboni humo, wameendelea kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa michango mikubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya usambazaji wa umeme kwenye vijiji vyote 68 vyenye jumla ya vitongoji 374 sambamba na kuipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri.
“Tunafurahi kuona Vijiji vyetu vyote vimeunganishiwa umeme pongezi kwa Mbunge wetu na Rais wetu pia kwa kazi nzuri za kutuletea maendeeleo. Na Sasa ni katika Vitongoji vyetu,hatua hii ni nzuri kwa maendeleo yetu Wananchi kupitia Nishati hii. Tutafanya kazi za ufundi ambazo zina hitaji umeme tutapata vipato vya kuhudumia familia zetu na kuinuka kiuchumi pia.”amesema Jefferson Mafaru.
Naye Fabian Maingu amesema kuwa iwapo Vitongoji vyote jimboni humo vikiunganishiwa Nishati hiyo, itawasaidia vijana wasiokuwa na ajira kujiajiri kupitia shughuli mbalimbali ambazo zina hitaji Nishati hiyo na hivyo kujikwamua kiuchumi.
More Stories
Wataalam Sekta ya utalii watakiwa kufanya kazi kwa uadilifu,kujituma na kuwa wabunifu
Shigongo: Rais Samia ameleta mafanikio mengi katika kukuza uchumi
Mpogolo amahukuru Dkt Samia