January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi washirikiana kuchangia ujenzi ofisi mpya ya CCM

Na Esther Macha, Timesmajira Online,Mbeya

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imekutana kwa lengo la kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ofisi mpya ya chama hicho.

Katika kikao hicho Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya,Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kushirikiana na Mbunge wa Lupa ,Masache Kasaka wameahidi kuchangia kiasi cha milioni 25(ishirini na tano) kila mmoja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo.

Huku Madiwani wa kila Kata kuchangia kiasi cha milioni mbili ili kukamilisha ujenzi wa ofisi mpya ya chama itakayokuwa na ukumbi wa mikutano sambamba na ofisi za jumuiya zote za chama.

Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chunya Noel Chiwanga na kuhudhuriwa na Kamisaa wa Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya Mayeka Simon Mayeka.