May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wafunguka juu ya utumishi uliotukuka wa Dkt Doto Biteko

Na David John timesmajira online Geita

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameacha alama kubwa katika Sekta ya Madini katika kipindi chote alichokuwa Waziri wa Madini na kupelekea mabadiliko makubwa katika sekta hiyo.

Hayo yamesemwa Septemba 23, 2023 na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wadau wa Sekta ya Madini wakati Dkt. Biteko akifungua rasmi Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini katika viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita.

Akizungumza mara baada ya salaam hizo Dkt. Biteko amesema kuwa masuala yote yaliyozungumzwa na mafanikio hayo katika Sekta ya Madini yametokana usimamizi madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye sekta hiyo.

Kuhusu Waziri wa Madini Anthony Mavunde amemtaka afanye kazi kwa bidii na kuwataka wadau wa Sekta ya Madini nchini kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake kila siku.

“Vision 2030, Madini Maisha na Utajiri itachangia kuleta mabadiliko na kupunguza umaskini kwa wananchi wengi nchini, Sekta hii ni moyo wa uchumi wa nchi tuitumie kikamilifu ili kuleta mabadiliko,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kununua kilo 400 za dhahabu zilizosafiswa katika viwanda vya ndani vya kuchenjua dhahabu nchini. Ameitaka Benki Kuu kuwaunga mkono wachimbaji wa madini nchini ili kuleta tija na kuongeza mchango wa Sekta ya Madini.

Kwa upande, wake Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa Dkt. Biteko ameifanya Sekta ya Madini imekua Sekta Kiongozi kwenye uchumi wa Nchi. Aidha ameipongeza mkoa wa Geita kwa kuandaa maonesho hayo kuwa yenye tija kwa wananchi wa mkoa wa Geita.

” Nimekuja na Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri ili hadi kufikia mwaka huo tuwe tumefanya tafiti katika eneo lote la nchi ya Tanzania ili wananchi wa waweze kunufaika na rasilimali madini,” amesema Waziri Mavunde.

Pia, amesema ifikapo mwezi Oktoba Serikali itakabidhi mashine tano za uchorongaji wa Madini