December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa Kanisa wamuomba Rais Samia kuingilia kati kupotea kwa Askofu Mkuu

Na Penina Malundo,timesmajira,Online

VIONGOZI wa  Kanisa la House of Prayer Shield of Faid Christian Fellowship lililopo maeneo ya Boko alimaarufu kanisa la Mzee wa Yesu,wakiongozwa na Mke wa Askofu wa kanisa hilo,Greener Mkombo waungana kumuomba  Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni,kuingilia kati suala la kupotea  kwa kiongozi wao ambaye ndio   Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Mulirege Kameka ndani ya siku saba.

Rai hiyo imetolewa leo  jijini Dar es Salaam na Mke wa Askofu huyo,wakati akiongea na waandishi wa habari kanisani hapo,amesema Askofu huyo,alikamatwa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji Mei 15,mwaka huu majira ya saa 2 usiku nyumbani kwao.

Amesema maofisa hao waliweza kuvamia nyumba yao na kumchukua Askofu huyo na kumleka katika ofisi za uhamiaji za kanda ya kinondoni ambapo hadi sasa wameweza kufatilia uwepo wa askofu huyo katika ofisi hizo wamekuwa wanajibiwa kuwa hayupo hapo.

“Tunaomba Rais Samia kuingilia sakata hilo  ili Askofu huyo aweze kuonekana na kama anakosa lolote amelitenda ni vema kupelekwa mahakamani kama sheria ya nchi inavyosema,”amesema na kuongeza

“Tumekuwa tukisumbuliwa na serikali juu ya uraia wa mzee tangu mwaka 2011 ambapo mwaka 2019 aliweza kushinda kesi na kupewa document na mahakama kuwa yeye ni raia wa Tanzania amezaliwa Mbeya Rungwe,mpaka leo hatujui Mzee yupo wapi tayari tumeenda Ofisi za Uhamiaji alipopelekwa wakasema hayupo,wanatupiana mpira tu,”amesema

Amesema nchi ya Tanzania chini ya Rais Samia tayari ameiweka  katika mstari mzuri unaoendana na sheria zake,hivyo kama Askofu huyo anakosa ni vema kufikishwa mahakamani au kama sio raia wa nchi hii arudishwe huko wanaposema ni kwao.

Naye Kiongozi wa Kanisa hilo,Nazar Temba amesema hadi sasa hawajui Askofu wao yupo wapi hivyo wanamuomba Rais Samia na Waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani kuingilia suala hilo.

Ameiomba Serikali iwawaeleze askofu huyo yupo wapi na kama siyo raia wa nchi hii basi anapaswa kupelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake dhidi yake.