December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi wa CCM wamjulia hali Prof.Jay

Na Penina Malundo,timesmajira,Online

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka kumjualia hali hali aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro na msanii nguli wa kizazi kipya Joseph Leonard Haule (Prof. Jay) alieyelazwa hospital ya Taifa Muhimbili akiendelea na matibabu.

Akizungumza baada ya kumjualia hali Prof.Jay,Chongolo amesema wamemuona Prof.Jay na hali yake inaendelea kuimarika huku wakiwashukuru Madaktari wa hospitali hiyo kwa huduma mzuri wanayoendelea kutoa.

“Tumemuona Ndugu yetu (Prof Jay) hali yake inazidi kuimarika, tumshukuru Mungu lakini niwashkuru madaktari kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kumhudumia, pamoja na mchango huu wa kuwezesha matatibu lakini kwa Niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan niwahakikishie tutaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha matibabu yanaendelea vyema huku tukiendelea kumuombea apone haraka” Amesema Chongolo.