November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Viongozi mbalimbali watoa baraka kwa Dkt.Tulia

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya

VIONGOZI wa dini,mila na Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya wametoa baraka kwa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini kuelekea kwenye uchaguzi ambapo anagombea kiti cha Uraisi wa Bunge la Dunia (IPU).

Baraka hizo zilitolewa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Suma Ikenda Foundation ya Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya Suma Fyandomo iliyofanyika katika ukumbi wa Landmark Tukuyu mjini.

Askofu Dkt Alex Malasusa Mkuu wa K.K.K.T Dayosisi ya Pwani amesema wajibu wa viongozi wa dini ni kuwaombea dua viongozi wa Serikali ili waendelee kupata mafanikio katika mambo mazuri wanayoyaanzisha hususani uanzishwaji wa taasisi za kusaidia jamii.

Aidha amesema viongozi wa Dini wanaoungana na watanzania kumuombea Dr. Tulia ili aweze kufanikiwa katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu ambapo anagombea kiti cha Uraisi wa Bunge la Dunia (IPU).

Naye Chifu Rocket Mwashinga kwa niaba ya viongozi wa mila amesema kazi yao ni kuhakikisha viongozi wa Serikali wanalindwa Ili wasipate na changamoto zozote.

Pamoja na kuhakikisha wanajenga umoja na mshikamano miongoni mwao na kupitia umoja huo Dkt. Tulia anaweza kufanikiwa kupata Uraisi wa Bunge la Dunia unia.

Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi amesema ni wajibu wa kila mkazi wa Mbeya kuhakikisha anamuombea mazuri Dkt. Tulia ili aweze kushinda uchaguzi huo kwani ushindi wake ni heshima kwa Taifa na Mkoa wa Mbeya bila kujali itikadi za kidini, rangi wala ukabila.