Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya
MWENEYKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge Nchini Mariam Nkumbi amewataka wananchi hasa vijana kujikita kwenye kilimo cha mkonge ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akziungumza kwenye maonyesho ya Nane Nane Jijini Mbeya amesema,Mkonge ni moja ambalo linavunwa kwa muda miaka 15 huku akisema linarahisisha mtu kujikwamua kiuchumi lakini ni zao ambalo mzazi anaweza kurithisha watoto wake.
Amesema,uwekezaji wa zao la mkonge ni mzuri maana ukishaupanda mkonge,ukianza kuvuna,unavuna kwa muda wa miaka 15.kwa hiyo naihamasisha jamii ijikite kwenye kilimo cha mkonge kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.”amesema Nkumbi
Amewaasa vijana kuacha kuzurura bila kazi na badala yake wajikite kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo katika kilimo cha mkonge ambacho kitawapatia kipato cha kujikimu wao na familia zao lakini kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
“Mkonge ni njia pekee ya kuwawezesha na kuwainua wananchi hususan vijana kiuchumi,ukipata eneo lako la zao mkonge ukawekeza katika kipindi cha miaka 15 wewe utakuwa unavuna tu.”amesisitiza
Vile vile amesema, kujikita katika zao hilo la mkonge na kumwezesha muhusika kupata mikopo ya riba nafuu kutoka benki itakayowawezesha kulima kwa tija.
“Hivyo mimi nawakarisha mpite kwenye banda letu mpate maelezo namna ya kufanya katika kulima zao hilo,na sasa hivi benki nyingi zinatoa mikopo ambapo mkonge ni zao mojawawapo ambalo benki inaliangalia katika kutoa mikopo kwa vijana hasa kwenye kilimo ambayo imeshushwa riba,”amesema
Amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kulima zao hilo la mkonge ambalo linastawi katika mikoa 16 hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya zao la Mkonge,Bodi ya Mkonge Tanzania Olivo Mtung’e amesema, lengo la Bodi ya Mkonge ni kuongeza matumizi ya mmea wa mkonge tofauti na sasa ambapo bado tunategemea matumizi ya bidhaa ambazo ni kama asilimia mbili tu.
Mtung’e amesema,wanahitaji kuongeza matumizi ya zao hilo hadi kufikia asilimia 50 kutoka na zao hilo kuwa na masoko makubwa ya mahitaji ya zao hilo ndani nan je ya nchi.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best