Na Joyce Kasiki, Geita
BALOZI wa Amani Tanzania, Mess Mbura, amesema juhudi za kuwawezesha vijana kiuchumi ni muhimu katika kujenga Tanzania yenye maendeleo, akieleza kuwa zaidi ya vijana 1,500 tayari wamesajiliwa katika mpango unaolenga kuwaunganisha na fursa za ajira na ujasiriamali.
Mbura amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Youth Foundation Tanzania katika maonyesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita .
Amesema mpango huo unalenga kuwasaidia vijana kupata ajira pamoja na kuwapa waajiri mbinu zinazoweza kuwawezesha kufikia mafanikio katika shughuli zao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Youth Foundation Tanzania, Yazidu Mtika, amesema taasisi hiyo inalenga kuwasaidia vijana kujitegemea kiuchumi kupitia mafunzo, elimu na kuwawezesha kutekeleza miradi yao.
Mtika amesema taasisi hiyo inatekeleza miradi katika sekta mbalimbali, zikiwemo madini, kilimo, uvuvi, teknolojia na ufugaji, huku ikiwakaribisha vijana kutoka sekta nyingine kushiriki.
Amesema taasisi hiyo inatarajia kukutana na vijana wa Mkoa wa Geita Oktoba 4 kwa ajili ya mafunzo ya uchumi na namna ya kuwawezesha vijana kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo yao.

More Stories
Makamu wa Rais ashuhudia moango wa Ufadhili wa Umeme
ESAP yaongoza huduma vilipuzi, uchimbaji Afrika Mashariki
Waziri Sangu aipongeza WCF na TRC