May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vijana wachangia maambukizi mapya ya VVU

Na Joyce Kasiki,Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera Bunge na Uratibu Jenista Mhagama amesema moja ya eneo linalohitaji msukumo na vipaumbele ni pamoja na kuimarisha afua za VVU na UKIMWI kwa vijana kutokana na hali ya maambukizi kwa kundi hilo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dodoma  kuhusu maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo kilele cha maadhimisho hayo kinatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro,Mhagama amesema, takwimu zilizopo zinaonesha kuwa, kundi la vijana wa umri wa miaka 15 hadi 24 linachangia maambukizi mapya ya VVU kwa asilimia 40 .

“Hali hii inalifanya kundi hilo kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi ya VVU,kwa mutakdha huo , maadhimisho ya mwaka huu yanatoa kipaumbele pia kwa vijana kushiriki kikamilifu kwenye majukwaa ya matukio yaliyoandaliwa kwenye maadhimisho haya kote nchini.”

Amesema hali hiyo ni mbaya na nguvu ya ziada inatakiwa kutumika ili kufanikisha na kuondoka katika athali zaidi kwa kushiriki kwenye majukwaa na midahalo mbalimbali yalioandaliwa kwenye maadhimisho hayo.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewata wanaume kujitokeza kupima Virusi vya UKIMWI kutokana na kubainika wazi jinsia ya kiume wako nyuma kushiriki suala zima la upimaji VVU na liwe zoezi endelevu.

Kwa mujibu wa Mhagama  wanaume wamekuwa wakiwategea wake au wenza wao na kusahau kuwa mwanaume anaweza kuwa na maambukizi ya UKIMWI na mkewe asiwe na maambukizi hayo. 

“Wanaume msitegee kwenda kupima afya zenu, msiwafanye wake zenu chambo kwenye suala zima la kucheki afya ,wote mnatakiwa kupima na kutambua hali zenu kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kufikia malengo ya kidunia na kuzifikia 95  tatu ifikapo 2030,” Amesema Waziri Mhagama 

Kwa upande wake Dkt.Anath Ruebembera Meneja Mpango wa Taifa wa kuthibiti UKIMWI,Wizara ya Afya amesema upatikanaji wa vipimo vya kupima VVU  vinapatikana kila mahali ikiwa ni pamoja na hospitali za serikali na sekta binafsi ambapo kwa sasa wameongeza  kipimo kingine cha kujipima mwenyewe baadae kwenda kuhakikisha kwenye vituo vya afya.

” Hivi sasa tutaweka utaratibu wa mtu wa kutokutumia kondom zaidi ya moja mwisho iwe kondom tatu  ili kila mtanzania imfikie maana wengine wamekuwa  wakichukua na kwenda kuuza”Amesema Dkt.Anath

Naye Makamu Mwenyekiti wa watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi VVU (NACOFA) Emanuel Msinga amesema kama taasisi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuwakusanya vijana kuanzia miaka 15 na kuendelea pamoja na vikundi vya kuhamasisha kwenye kata na wilaya ambapo ni mfano hai ndani ya miaka mitatu