May 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Vijana wa Kitanzania kupatiwa mafunzo kidijitali

Na Bakari Lulela,Timesmajira

VIJANA wa kitanzania wapatao 5000 kupatiwa mafunzo elekezi ya kidijitali katika masuala ya kiuchumi, uongozi na kibiashara Ili kuwa wafanisi katika uwajibikaji.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na Mlezi wa Vijana na Mkurugenzi wa Shirika laTanzania Bora imIntative Abella Bateyunga ambapo amesema program hiyo imekuja kuwafikia vijana wa rika la miaka 16 mipaka 25 katika masuala ya kijinsia.

“Programu hii ni umuhimu kwa usawa wa kijinsia kwa makusudi mbalimbali ya vijana waume kwa wake yenye lengo la kuwaelimisha vijana mambo mbalimbali ikiwemo kujiajiri sambamba na kuitafuta fursa wezeshi za kujipatia maendeleo,” amesema Bateyunga

Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa lengo la kuwakutanisha makundi ya vijana ni pamoja na kuwaelimisha katika masuala ya uongozi sambamba na kuziendea fursa mbalimbali za ajira rafiki ambazo ni muhimu Kwa makundi ya vijana wa kitanzania.

Mafunzo hayo ni mahsusi kwa vijana wa miaka 16 hadi 25 ambapo baadaeni watakuwa mabalozi wazuri kwa makundi mengine ya vijana katika masuala ya kulitumikia Taifa lao.

Hata hivyo Tanzania Bora intative inakuwa na vijana katika kuwapa uwezo wa wao kujitambua katika kuyaendea masuala mbalimbali ya maendeleo ndani na nje ya jamii yetu.

Mradi huu unawawezesha vijana wa kitanzania kuwa na mawazo chanya katika kulinda na kudumisha amani ya nchi kwa kuzingatia uongozi Bora ndio suluhisho la matattizo mbalimbali ikiwemo uonevu, Rushwa, Haki za binadamu.