December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Mkuu wa Bunge, Stephen Kigaigai akiongea na waandishi wa habari katika Banda la Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (Veta).

Veta watakiwa kuongeza Ubunifu

Na Penina Malundo,Times Majira Online, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Bunge Stephen Kigaigai ameitaka Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), kuongeza ubunifu na kuwaimarisha zaidi vijana katika masuala ya ufundi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, katika maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, wakati akitembelea banda la mamlaka hiyo, Kigaigai amesema wizara ya elimu inapaswa kuweka msisitizo kwa Veta kuhakikisha vijana wanaohitimu masomo yao wanawafuatilia ili kutowapoteza katika ufundi wao.

Amesema, pia ifanyike ufuatiliaji wa kuangalia vijana wanapomaliza Veta wanaenda wapi na wanaendeleza vipaji vyao vipi.

“Veta na Wizara ya Elimu wanatakiwa kushirikiana kuwafuatilia vijana hawa wanapomaliza masomo yao wanakwenda wapi na wanafanya nini. Kama taifa iwapo itatumia wataalamu kutoka Veta nchi itafika mbali,” amesema.

Amesema, Veta yenyewe ni kiwanda kwani wamekuwa wakizalisha Wataalam mbali mbali ambao wengi wao wanaajiliwa katika viwanda na pamoja na kujiajili wenyewe.