Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) Makao Makuu imetengeneza teknolojia ya udongo wa kuoteshea mazao ya bustani na mbogamboga ili kumpunguzia mkulima gharama za kilimo na hivyo kuleta tija kwenye sekta ya kilimo na jamii kwa ujumla.
Udongo uliopo nchini kwa sasa kwa ajili ya shughuli hiyo unatoka nje ya nchi hivyo mkulima huupata kwa bei ghali .
Akizungumza kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji 88 viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ,Afisa Ufuatiliaji na tathimini ya Mafunzo Makao Makuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Joseph Kimako wameamua kuja na teknolojia hiyo kutokana na udongo wa aina hiyo unaouwa hapa nchini unatoka nje ya nchi na kwa gharama kubwa.
“Teknolojia hii ni rahisi ambapo tunachukua udongo wa msituni tunachanganya na samadi ya ng’ombe na pumba za mpunga na baada ya hapo tunawekwa kwenye mtambo unaochemsha maji ili kuua masalia ya magugu na wadudu.”amesema Mhandisi Kimako
Amesema udongo kama huo unaouzwa kwenye maduka ya pembejeo unatoka nje ya nchi lakini virutubisho vinavyopatikana ndani yake ,vipo kwenye malighafi zinazopatikana hapa nchini.
“Kwa hiyo hili ni moja ya zao ambalo linapatikana kwenye fani zetu tatu za kilimo tunazozitoa VETA ambazo ni fani ya zana na mitambo ya kilimo ,fani ya mazao ya bustani na fani ya uzalishaji kwenye kilimo.”amesisitiza Mhandisi huyo
Kwa mujibu wa Mhandisi Kimako ,wameamua kuja na hiyo teknolojia kwa sabahu udongo wa kuoteshea mazao ya bustani na mbogamboga ukienda kwenye maduka ya pembejeo unatoka nje ya nchi na unauzwa kwa bei ghali .
Amesema,wameamua kutengeneza teknolojia hiyo ili kumsaidia mkulima aweze kupata mafunzo ya kutengeneza udongo huo ili waweze kulima kilimo chenye tija.
Amewashauri wakulima waende VETA kujifunza namna nzuri ya kutengeneza udongo huo ili kupunguza gharama za kwenye kilimo lakini mwisho wa siku wataenda kulima kilimo chenye tija na hivyo kupata faida kubwa kwenye kilimo.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu