January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uzinduzi wa Albam ya ‘Bila Chanzo Halisi Hutoboi’

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

KANISA Halisi wamezindua Albamu ya bila chanzo Halisi Hutoboi, ikiwa ni sehemu ya pili ambapo Albamu hiyo imebeba nyimbo 12

Sehemu ya kwanza ya Albamu hiyo ilizinduliwa katika kanisa Halisi lakini sehemu ya pili Albamu hiyo imezinduliwa nje ya kanisa la Halisi

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam kiongozi wa kanisa hilo, Amani Halisi alisema katika kanisa hilo wamekuwa wakifundisha amani kwa wote, ibada, upendo uliopitiliza, kufanya kazi na jamii inayotuzunguka

“Tuko hapa ili watanzania wajue kuwa kanisa Halisi lipo kwaajili yao”

Aidha alisema mapokeo ya uzinduzi wa Albamu hiyo yamekuwa ni makubwa tofauti na awamu ya kwanza kwani takribani mataifa 7 yameshiriki na kusikilizwa na mataifa 130 Duniani.

“Mapokeo ni makubwa sana kwasababu leo tupo nje ya kanisa ambapo mataifa takribani 7 yameshiriki na tunasikilizwa na mataifa 130 Duniani, ndani ya makanisa ya Tanzania tuna makanisa 360”

Kuhusu Mchango wa Serikali, Amani alisema wameendelea kushirikiana nao bega kwa bega ambapo inapelekea Wana Halisi kwa ujumla kuendelea kuwafanyia maombi viongozi wote wa serikali.

“Mchango wa serikali inatupenda maana tunafanya kazi na serikali katika majira ya nyuma wenzetu waliopita hawakufanya kazi na serikali mfano Musa hakufanya na farao n.k, ila sisi kanisa Halisi tunafanya kazi na serikali na ndiyo maana Kila siku tunafanya maombi maalumu kwaajili ya  serikali yetu”

Naye mtekeleza sauti lango Moja la mafanikio, kutoka kanisa la Halisi Mkoa wa Tanga aliwataka Wana Halisi waendelee kumuabudu muumbaji kwani ndiyo kusudi la aliyewaumba.