March 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UWT Tabata watakiwa kuhamasisha uandikishaji daftari la mpiga kura

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Dar

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),kutokea UWT Wilaya ya Ilala Salima fumbwe , amewataka wanawake wa UWT Kata ya Tabata,kuhamasisha watu kujiandikisha katika maboresho ya Daftari la Mpiga Kura zoezi linaloanza leo Machi 17,2025.

Fumbwe amesema hayo Kata ya Tabata wakati wa mkutano wa wanawake kwa ajili ya kutoa elimu ya kushiriki katika zoezi la maboreshe na kujiandikisha katika Daftari la Mpiga Kura uliandaliwa na UWT Kata ya Tabata, ambapo zaidi ya wanawake 500 walishiriki.

Ambapo amewataka wanawake hao kusimama imara kuhamasisha watu kuanzia ngazi ya mashina na familia zao wakashiriki kujiandikisha ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu na kuiwezesha CCM kuendelea kushika dola.

Sanjari na hayo amewataka UWT,kutembea kifua mbele na kusemea maendeleo ya Kata ya Tabata yaliofanywa na Serikali pamoja na kuwathamini wanawake wa Tabata na kujenga umoja na mshikamano.

Mwenyekiti wa UWT kata ya Tabata Zena Kengera,amewataka wanawake wa UWT Tabata, kujenga umoja na mshikamano na muda ukifika waweze kumpigia kura za kishindo mwanamke mwenzao Dkt.Samia Suluhu Hassan.