September 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UWT Ilala yawataka wanawake wasitumike kisiasa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala imewataka Wanawake wa UWT wasitumike KISIASA Viongozi waliopo madarakani wanatosha badala yake wametakiwa kuwapa ushirikiano katika kujenga chama na serikali.

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Wilaya ya Ilala Neema Kiusa, alisema hayo Kata ya Segerea ,Jimboni la Segerea Wilayani Ilala wakati wa Baraza la UWT Kata ya Segerea .

“Nawaomba Wanawake Wenzangu wa kata ya Segerea tunatakiwa kujenga ushirikiano umoja Katika kujenga chama na Jumuiya zetu Viongozi waliopo madarakani kwa Sasa wanatosha wapewe ushirikiano msikubali kutumika KISIASA wakati wa uchaguzi bado ” alisema Neema .

Mwenyekiti Neema amewataka Wanawake wa Wilaya ya Ilala wafanye Siasa safi na kufuata kanuni za chama na Jumuiya kwani wao ni Jeshi Imara Katika kukipigania chama Katika chaguzi mbalimbali .

Aliwataka wafanye ziara na kutembelea makundi maalum pamoja na kukitangaza chama katika Ilani ya utekekezaji kwa kumsemea Rais wa Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika miradi ya Maendeleo ikiwemo Sekta ya Elimu ,Afya ambapo Rais amefanya mambo makubwa hivyo tutembee kifua mbele .

Aidha aliwataka washirikiane kwa pamoja Muda wa kufanya kazi waache nongwa za kisiasa wote ni wamoja Sasa hivi ni wakati wa kujenga Jumuiya na kuingiza Wanachama wapya kadi zipo za kutosha Wilayani.

DIWANI wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Batuly Mziya aliwataka Wanawake wa UWT wajiandae kuchukua fomu kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika kusaka Dola .

DIWANI Batuly alisema CCM ni Jeshi kubwa Wanawake wanaweza kuongoza nyazifa mbalimbali za uongozi hivyo watumie fursa hiyo katika kugombea Dola kwani wanatosha .

DIWANI Semeni Mtoka aliwataka Wanawake kuwa wamoja kushirikiana kuunda vikundi vya ujasiriamali waweze kutambulika katika mikopo ya Halmashauri ya Wanawake Vijana na watu wenye ulemavu .

DIWANI Viti Maalum Magreth Cheka aliwataka UWT Segerea kusaka Wanachama wapya katika kujenga chama na Jumuiya katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025 wa wabunge na Rais.

Mlezi wa Umoja Wanawake Segerea DIWANI Julieth BANIGWA aliwataka UWT kuweka mikakati ya ushindi kwa kufungua matawi ya UWT kila shina pamoja na kukagua miradi ya Serikali pamoja na kukisemea chama .

Katibu wa Umoja wanawake Kata Segerea Fatuma Issa akikabidhi zawadi ya mayai Kwa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa Katika baraza la uwt Segerea Picha na Heri Shaaban.
Mwenyekiti wa Umoja wanawake Wilaya ya Ilala Neema Kiusa akizundua Baraza la UWT Segerea Kwa kukata keki maalum katika balaza Hilo (Picha na Heri Shaaban )
DIWANI wa Viti maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Batuly Mziya akizungumza Katika baraza la Wanawake Kata segerea (Picha na Heri Shaaban )
DIWANI wa Viti maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Semen Mtoka akizungumza katika baraza la uwt Kata ya Segerea (Picha na Heri Shaaban )
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa akizungumza na Wanawake wa UWT Kata ya Segerea wakati wa kuzindua baraza la uwt (Picha na Heri Shaaban.