Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MSANII wa filamu hapa nchini mwenye mvuto wa aina yake Irene Uwoya,leo ametambulisha rasmi bidhaa zake atakazoziuza kwenye Maonesho ya Biashara kwenye viwanja vya Sabasaba Temeke, Dar es Salaam.
Akitambulisha bidhaa hizo kupitia kwenywe Ukurasa wake wa Instagram, Uwoya amesema kupitia Kampuni yake ya I Cosmetic anafarijika sana kutumia fursa ya ‘Meet your Star’ iliyozinduliwa jana ili kutangaza bidhaa zake.
“Kabla ya Ufunguzi Rasmi ambao unakuja, napenda kutambulisha Product yangu mpya kabisa ya urembo kupitia kampuni yangu ya I COSMETICS, nafarijika kutumia Platform ya ‘Meet Your Star’ Sabasaba kama sehemu yangu ya kwanza ambayo unaweza kuipata Product hii, na hii ni kwakuwa nathamini Mashabiki wangu ambao ndio wamekuwa Nguvu yangu muda wote.
“Karibu Sabasaba kwenye Mabanda ya ‘Meet Your Star’ uje kujaribu Product hii huku mimi nikikueleza faida zake na matokeo
“Tuna Brightening Body Lotion, Brown Skin Lotion, Face Cream, Mens Essential, Brightening Serum na Anti Aging Serum, na jina linalobeba Product zote hizi ni Renee.Unavyoniona mimi ni matokeo ya Product hizi na ndizo ninazotumia,” amesema Uwoya.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio