Na Penina Malundo, Timesmajira
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.
Taarifa iliyotolewa kwa umma na Mamlaka hiyo Leo,imesema mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla ya
kuanza kupungua nguvu.
Imesema kuwa kutokana na umbali kutoka nchini, kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja katika kusababisha ongezeko la mvua nchini.
Taarifa hiyo imesema vipindi vya upepo mkali na
mawimbi makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi.
“TMA inatoa ushauri kwa watumiaji wa bahari na Wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatiabtaarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya hali ya hewa nchini pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta,”imesema
Aidha TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba