NA
K-VIS BLOG, LINDI
MFUKO
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma PSSSF, umetoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa 7 wa Jukwaa la Wahariri Tanzanai (TEF) mjini Lindi.
Akizunguza
leo Novemba 14, 2023, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James
Mlowe, amesema hadi kufikia Septemba 2023, uwekezaji wa Mfuko umefikia zaidi
ya shilingi Trilioni 8.16.
Amesema
mafanikio hayo ya uwekezaji ni ya kujivunia kwani ni makubwa ndani ya kipindi kifupi na yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi
kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wake, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuongeza
ajira, kufungua nchi na kuboresha mazingira ya uwekezaji.
Kwa
upande wake Meneja Mafao wa PSSSF, Bw. Ramadhani Mkeyenge, amesema ukiacha
jukumu hilo la Mfuko katika eneo la uwekezaji, Mfuko pia umetekeleza kwa
mafanikio makubwa jukumu la Ulipaji Mafao.
Alisema
Mfuko unatoa jumla ya Mafao saba (7) ambayo ni pamoja na Fao la Uzeeni
(Pensheni), Fao la Ulemavu, Fao la Kifo, Fao la Urithi, Fao la Uzazi, Fao la
Kukosa Ajira na Fao la Ugonjwa.
Mfuko
unalipa pensheni kwa Wastaafu 167, 937 na Wategemezi, wastani wa shilingi
bilioni 67 kila mwezi.” Alifafanua Bw. Mkeyenge
“Mfuko tangu uanze kutekeleza majukumu yake mwaka 2018 hadi Juni 2023, umelipa kiasi cha shilingi trilioni 8.8 kwa wanachama wapatao 262,095.” Alisema na kuongeza…Kila mwezi pensheni inayolipwa kwa wastaafu na wategemezi ni wastani wa shilingi bilioni 67.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), akimkabidhi cheti cha shukrani, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), akimkabidhi cheti cha shukrani, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, PSSSF, Bw. James Mlowe.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria