Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Rukwa
Wananchi wa kijiji cha Swahila kata ya Mkwamba wilayani Nkasi wameridhishwa na uwazi unaofanya na viongozi wao wa Kijiji katika kuweka wazi mapato na matumizi kitu kinachowafanya wao kujitokeza katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijiji.
Wakizungumza na Timesmajira Online wananchi hao walisesema kuwa hivi sasa wanajenga shule mpya ya msingi shikizi kwa njia ya kujitolea,kuongeza ukubwa wa jengo la zahanati ya kijiji hicho pamoja na kuwa tayari kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha shughuli hizo.
Baadhi ya wananchi hao akiwemo Sophia Kambaulaya na Judithi Kipeta,wamesema wameguswa na utaratibu wa kujitolea kwenye shughuli za maendeleo kutokana na uwazi uliopo wa viongozi wao,ambao wamekuwa wakiwasomea mapato na matumizi kila wakati na kazi inayofanyika inaonekana.
Walisema kuwa kwa utaratibu huu ambao haukuwepo hapo nyuma umewatia nguvu kubwa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo,hivyo utasaidia kujiletea maendeleo kwa haraka.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Legius Choma amekiri kuwepo kwa kasi ya wananchi kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo huku akibainisha kuwa siri ni uwazi wa michango wanayoitoa ikiwa ni pamoja na kazi inayofanyika kuonekana.
Amesema kuwa wao kama viongozi wa Kijiji waligundua kuwa kutokuwepo kwa uwazi wa michango umekuwa kikwazo cha muda mrefu kwa wananchi kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo.
More Stories
Prof.Mbede:Nishati ya umeme wa Sola imepunguza vifo vya wajawazito
Rais Samia apongezwa kuanzisha bima ya afya kwa wote
Serikali yajipanga kudhibiti matumizi yasiyo sahihi kuelekea uchaguzi mkuu