Na Bakari Lulela,Timesmajira
UMOJA wa vijana wa CCM Taifa umezindua program maalumu ya kijani ilani chatbot kwa lengo la kusaidia kutambua mchakato mzima wa uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika octoba 2025 nchini kote
Program hiyo wezeshi itakuwa ikielekeza namna ya kupata taarifa mbalimbali kwa usahihi mkubwa zinazohusiana na uchaguzi huo bila kubagua upatikanaji wa kura, namna ya upangaji wa wagombea kwenye maeneo yao.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kijani ilani chatbot mgeni rasmi katika tukio hilo mwenyekiti wa uvccm Taifa Mohammed Kawaida amesema kwamba tukio hilo ni muhimu kwa wananchi, wanaccm kubaini kipi kimefanyika katika mchakato wa kupata matokeo kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
“Mimi nianze kwa kumshukuru mungu kwa kutujalia uzima na kumshukuru muheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kumsindikiza kuchukua fomu hivyo pia tunataka vijana na wanachama ifikapo octoba 29 mfike kwenye vituo kwa ajili ya upigaji wa kura,” amesema Kawaida
Kawaida amesema kwakumpongeza Katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa CCM Ally Mwinyi aliyechaguliwa jijini Dodoma kushika nafasi hiyo na kusisitiza kuwa waende wakatumie program hiyo ya chatbot vizuri ambayo itasaidia sana kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa umoja wa vijana Taifa uvccm Ally Mwinyi amesema kuwa anakishukuru chama cha Mapindizi kwa kumpa dhamana na kamati kuu ya chama na kuahidi kuwa mtii na kumshukuru mwenyekiti wake Mohammed Kawaida na kumshukuru mtangulizi wake Joketi Mwengelo napenda kuwashukuri wateule wenzangu
Tumekusanyika hapa kuzindua mfumo wetu maalumu Ili iweze kufanya kazi mbalimbali kuuliza maswali mbalimbali lengo kuu la chama ni kushika Dola pande Zote kwa maana bara na Zanzibar ni jukumu letu vijana tuendelee kuhamasishana Ili tuweze kumchagua Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwa kiwango cha juu.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako