January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UVCCM Dar es Salaam yawaomba wananchi kumuunga mkono Rais Samia

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), mkoa wa Dar es Salaam, umewaomba wananchi wenye mapenzi mema na nchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia na serikali ya CCM anayoiongoza kwani amekuwa kiongozi msikivu na mzalendo kwa maendeleo ya taifa.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam leo na Mwenyekiti wa UVCCM, mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohamed wakati akitoa tamko juu ya mjadala wa kuridhia kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii wa uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Nasra amesema watanzania waendelee kumuunga mkono kwa sababu amejidhihirisha kuwa anao uwezo wa kuwaongoza na kusikiliza kero mbalimbali za Watanzania

“Uamuzi alioufanya Rais Dkt Samia umewagusa vijana hao kwa kuzidi kuonesha ni kiongozi msikivu kwani kipindi cha nyuma palikuwa na malalamiko kwa nini serikali haipeleki mikataba inayohusisha uwekezaji mkubwa wenye maslahi mapana ya nchi bungeni”amesema

Amesema imedhihirisha kuwa ukomavu wa uongozi, umahiri na umakini wa Rais Dkt. Samia, hivyo wanampogeza tunampongeza kwa
kwa kuoneonesha kwa dhati kwa kauli na vitendo kuwa yeye ni mwanademokrasia makini kwa kuwa na uongozi mahiri anayewasikiliza wananchi wake akithibitisha kwa kusema na kutenda.

“Rais Dkt Samia yupo tayari kupokea na kusikiliza maoni mbalimbali, kushauriwa na kukosolewa kwa hoja sio matusi , hivyo tunawataka wanasiasa waliofilisika hoja wasitumie udemokrasia wa Rais Dkt Samia vibaya kuvuruga amani na utulivu na kusababisha taharuki kwa kutoa kauli ambazo ni hatarishi nchini.