December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ushindi wa Yanga dhidi ya Simba wamfurahisha Uwoya

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

USHINDI wa juzi walioupata klabu ya Yanga dhidi ya watani wao wa jadi Simba, umemfurahisha msanii wa filamu hapa nchini mwenye mvuto wa aina yake Irene Uwoya.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania uliochezwa juzi kwenye Uwanja Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga waliibuka na ushindi wa goli 1-0, lililofungwa na kiungo Zawadi Mawia.

Akiongea kwa furaha kupitia kwenye UKurasa wake wa Instagram Uwoya amesema, hajawahi kujuta hata siku moja kuipenda Yanga kwani huwa inampa faraja isiyo kifani.

“Sijawahi kujuta na sitakaaa nijute kuipenda yanga.Mmejua kunipa raha, sasa mashabiki wadamu wayanga leo nitaokutana nao mtafurahi,” amesema Uwoya.