Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZAZI na walezi wameshauriwa kupeleka watoto chuo cha VETA kujifunza fani ya useremala ili waweze kujiajiri,kuajiriwa na kuajiri watu wengine na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Mwalimu wa fani ya useremala Chuo cha VETA Mkoani Tanga Yusufu Mkahala ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Amesema,hiyo ni fani mama kwani mahitaji ni mengi kwa matumizi katika jamii kwa hiyo uhitaji ni mkubwa hasa wa samani kuanzia nyumbani ,shuleni hadi maofisini.
“Katika useremala unaweza kuzaliwa masikini lakini siyo lazima kufa masikini kwa sababu ukiwa na fani hiyo una uwezo wa kufanya kazi bila oda ya mtu yeyote na ukabuni kitu kizuri chenye mvuto kwa watu na watu wakanunua.”amesema Mwalimu Yusuf
Amesema kuwa ukiwa na fani hiyo ni rahisi kujiajiri na kwamba unapopata wateja wengi zaidi ni rahisi kuajiri wengine ili kukamilisha kazi za wateja ulizo nazo.
Amesema fani hiyo ni muhimu katika kutatua changamoto ya ajira kwani uwezekano wa kujiari,kuajiriwa ama kuajiri wengine ni mkubwa unapokuwa na fani hiyo.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria