April 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

USAID, WFP wasaidia wakimbizi Kigoma

Na David John, TimesMajira Online

SERIKALI ya Marekani kupitia shirika lake la Maendeleo la kimataifa USAID limekabidhi msaada wa tani 12000 za Unga Mahindi zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 9 kwa shirika la mpango chakula Dunia WFP kwa ajili kusaidia kambi mbili za wakimbizi mkoani Kigoma.

Akizungumza katika makabidhiano hayo ambayo yamefanyika katika Ofisi za WFP Jijini Dar es Salaam Balozi wa Marekani hapa Nchini Donald Wright amesema msaada huo mpya utawezesha ushirikiano kati ya Shirika la USAID na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Chakula Duniani WFP.ili kutoa msaada wa chakula kwa ajili ya kuokoa maisha ya wakimbizi 204000.

Amesema wakimbizi ambao wamehifadhiwa kwenye kambi zilizopo kaskazini Magharibi mwa Tanzania nakwamba anaamini msaada muhimu wa chakula ili kuleta unafuu wa haraka kwa watu wanaioshi katika mazingira magumu.

”Tunashukuru kwa usaidizi huu unaondelea na unaotolewa kwa wakati kutoka Marekani ”alisema Sarah Gibson ambaye ni mkurugenzi mkazi na mwakilishi wa WFP nchini Tanzania

Ameongeza kuwa ” mchango huu ni muhimu si kwasababu ya thamani ya chakula kwenda kwa wakimbizi lakini pia kwasababu ya matokeo chanya yatokjanayo na ununuzi wa chakula ndani ya nchi.

Sarah amesema kuwa WFP imekabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha tangu mwaka 2020 uliopelekea kupunguza kwa mgao hadi asilimia 68 chini ya mahitaji .kwani kupunguza kwa mgao kwa muda mrefu unahatarisha ulaji wa chakula,lishe na afya ya wakimbizi.

Ameongeza kuwa licha ufadhili huo mpya, WFP bado haiwezi kutoa mgao kamili kwa wakimbi kutokana na uhaba wa fedha unaohusiana na kiwango wa idadi ya majanga kibinadamu duniani kote nakwamba USAID ndio mfadhili mkubwa zaidi ya upereshani ya WFP ya wakimbizi nchini Tanzania ambapo inatoa theluthi moja ya bajeti yao ya kila mwaka.

”Tangazo la leo la dola za Marekani milioni 9 ambazo ni nyongeza ya dola za Marekani milioni 4 zilizotolewa USAID kwa WFP Februali 2022 zinatatumika kununua zaidi ya tani 12,000 za unga wa mahindi na kuingizwa kwenye kikapu cha mgao wa chakula kinachosaidia wakizmbizi wanaoishi katika kambi mbili za wakimbizi nchini

katika hatua nyingine Balozi huyo wa Marekani nchini ameitaka Serikali ya Tanzania kuhaskikisha mahitaji ya kibinadamu ya wahamiaji wote wanaoishi katika magumu yanafikiwa.

Kwaupande wake mkuu wa ofisi ya WFP Kasuru Nyanzobe Malimi Ameshukuru msaada huo walioupata kwani zaidi ya watu laki mbili wanategemea chakula cha WFP nakwamba fedha hizo zilizotolewa na Marekani zimenunua chakula kwa wakulima wa Tanzania.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright (Kulia) akipika ugali kama ishara ya kupokelewa kwa msaada wa unga wa mahindi tani 12000 zenye thamani ya dola za Marekani milioni tisa ambazo wamekabidhi kwa shirika la Mpango wa chakula duniani(WFP) leo Juni 30,2022.Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Sudi Mwakipesi na kushoto ni Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Sarah Gordon-Gibson.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright (Kulia) akikabidhi mfuko wa unga wa mahindi kwa Mkurugenzi mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Sarah Gordon-Gibson (Katikati) wakati wa makabidhiano ya msaada wa unga wa mahindi tani 12,000 zenye thamani ya dola za Marekani milioni tisa kwa ajili ya wakimbizi wanaoishi katika kambi mbili za wakimbizi mkoani Kigoma.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka wizara ya Mambo ya Ndani Sudi Mwakipesi.