Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Aliyekuwa diwani wa Kunduchi ambaye alikatwa jina lake na wananchi kuandamana hadi ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM), Michael Urio ameongoza kwenye kura za maoni za udiwani katika kata hiyo ya Kuduchi.
Kura hizi ambazo zilizopigwa jana Agosti 4, 2025 ambapo jumla ya kura zote za kata ya hiyo zilikuwa 789 na Urio ameongoza kwenye Kata ya Kunduchi kwa kura 257, nafasi ya pili ni Joyce Haule 250, Emmanuel Mkuchu 240, Hashim Komba 30, Happiness Kinyaha 12.
Jana Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Jacob Siayi amesema jimbo la Kawe lina kata 10 ambazo zilishiriki katika upigaji kura wa udiwani.
Katika kata ya Kawe kura zilizopigwa ni 835 huku diwani aliyekuwa anatetea nafasi yake Mutta Rwakate ameshika nafasi ya pili kwa kura 307 nyuma ya Bernard Malima mwenye kura 327, akifuatiwa na Salun Kuhowa 162, Asha Komba 26 na Othaman Kipeta 12.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako