Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Simanjiro
Upepo mkali ulioambatana na mvua umezua taharuki katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara,baada ya kuezua paa za nyumba, sehemu za biashara za vinywaji ( Bar ),pamoja na kijiwe cha kuuzia magazeti.
Akizungumza na Majira Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani,Hans Nkya,amesema,ulianza upepo kisha ukaambatana na mvua, umesababisha taharuki kwa wakazi wa Mji huo.
Huku akitaja baadhi ya sehemu zilizoathirika zaidi kuwa ni pamoja na maeneo ya sheli ya Panone , ambapo mti mkubwa umeangushwa na upepo huo mkali,ambapo kilikua kijiwe kikuu cha uuzwaji wa magazeti.
” Eneo lingine ni la kuoshea magari ( Car Wash), maarufu kwa Mzee Simango, ambapo paa limeezuliwa na upepo huo,”.
Eneo lingine lililoathirika na upepo huo ni sehemu ya biashara ya vinywaji ( Bar) Liverpool Kata ya Mirerani.
Sanjari na hayo amewa tahadharisha wananchi kutokukaa karibu na miti pamoja na kuangalia paa za nyumba zao kama zimekaa vibaya waweze kuzirekebisha,kwa ajili ya tahadhari na usalama.
More Stories
Mashirikisho yaunga mkono azimio mkutano mkuu CCM
Watumishi wa Mahakama waonywa
CCM ilivyotambua mchango wa wanahabari Mkutano Mkuu Maalum