Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dar
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amepongeza utayari na mshikamano, uliooneshwa na Watanzania mara baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa,eneo la soko la Kariakoo,jijini Dar-es-Salaam.
Amesema,hatua hizo zimeonesha uzalendo na moyo wa udugu uliojengwa ndani ya Taifa la Tanzania.
“Shughuli za uokoaji zilianza mara moja, zikiongozwa na wananchi wa kawaida. Hii inaonesha moyo wa Utanzania wa kweli, ambapo unapomwona mwenzako kwenye shida, unaacha kila kitu na kumsaidia. Nawashukuru kwa moyo huo wa kipekee,”amesema Balozi Nchimbi.
Akizungumza, Novemba 17, 2024, alipotembelea eneo la tukio, Balozi Nchimbi alitoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na kuwafariji majeruhiwa.Ambapo amesitiza umuhimu wa mshikamano katika nyakati za dharura.
“Kwa namna ya pekee, napenda kutoa pole zangu za dhati kwa familia za wenzetu waliopoteza maisha, maisha ya kila Mtanzania yana thamani kubwa.Tunaomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi,” amesema Balozi Nchimbi na kuongeza:
“Majeruhiwi walioko hospitali na waliotoka, tunawaombea uponaji wa haraka na Mwenyezi Mungu awajalie nguvu na afya njema ili muweze kurejea katika shughuli zenu,”.
Aliongeza kuwa juhudi za vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi binafsi na wadau wengine zinapaswa kupongezwa kwa moyo wa kujitolea.Hivyo amesisitiza kuwa CCM,inaunga mkono juhudi za uokoaji na kipontayari kutoa usaidizi unaohitajika.
“Uokoaji huu haupaswi kusimama kila maisha yanahesabika, kama chama, tupo tayari kushirikiana ili kuhakikisha watu zaidi wanaokolewa,” .
More Stories
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa