Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Hayo yalielezwa jana na Mratibu wa wa afya ya mtoto wizara ya afya na mkuu wa kitengo cha afya ya uzazi Felix Bundala wakati akipokea vifaa vya uzazi vilivyokabidhiwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshuhulikia maswala ya afya ya uzazi na idadi ya watu (UNFPA) kwa serikali ya Tanzania na kuongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuwajengea uwezo watoa huduma kupitia mifumo ya kieletroniki kwani afya ya uzazi na mtoto ni muhimu na malengo ni kuhakikisha wanapunguza mimba za utotoni, vifo vya uzazi na vifo vya watoto.
“Pamoja na kwamba ni lazima miongozo na sera iliyopo lakini watoa huduma wenye ujuzi na wanaojitosheleza ni kitu kingine cha umuhimu na hawawezi Kufanya shughuli kama hakuna bidhaa muhimu ikiwemo vifaa tiba hivyo wizara inawajibu kuhakikisha miongozo kuwepo na wadau wetu wanaweza kuunganishwa vizuri katika kusaidia rasilimali mbalimbali ambazo zinahitaji”Alisema Bundala na kuongeza kuwa;
Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa UNFPA Mark Brian Schreiner alisema tangu mwaka 2015 mpka 2021 UNFPA na jumuiya ya madola ya uingereza FCDO zimenunua asilimia 53 za bidhaa za afya ya uzazi nchini Tanzania ambazo thamani yake ni dola za kimarekani milion 54.2 na kwamba matarajio yao ni kuwa zitapunguza mimba zisizotarajiwa milioni 9, zitazuia vifo vya uzazi karibu milioni moja na pia utoaji wa mimba usio salama milioni 2 hali itakayosaidia kuokoa dola za kimarekani milioni 756 katika huduma za moja kwa moja za afya.
Naye mkurugenzi ofisi ya maendelo ya uingereza kimataifa na jumuiya ya madola Kemmy Williams alisema utafiti wa demografia nchini kwa mwaka 2010 ulikadiria kuwa na asilimia 26 ya watoto walizaliwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya utafiti hawakuwa wametarajiwa.
Aidha mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Mavere Ally Tukai alisema wao kwa nafasi yao watahakikisha vifaa tiba hivyo vilivyopokelewa vinahifadhiwa katika mazingira mazuri ili kuwafikia walengwa waliokusudiwa na kuongeza kuwa kwa kushirikiana na wizara ya afya watahakikisha wanafikia malengo ya kutatua changamoto za kiafya kwa mtanzania;
“Bidhaa zilizopokelewa leo tutazihifadhi sehemu sahihi na tutazisambaza zinapotakiwa kwenda na vilevile kila kilichosambazwa kinatakiwa kuripotiwa kwamba kimefika na endapo kama kunachangamoto yoyote itabidi taarifa itolewe ili kufanyiwa marekebisho lengo ni mtanzania apate anachostahili kwenye upande wa bidhaa za Afya ili kutatua changamoto za kiafya”
More Stories
Balozi Kombo :Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu nishati yakamilika, Marais 25 kuhudhuria
Mbunge Mavunde awawezesha kiuchumi wafanyabiashara soko la Sabasaba Dodoma
Msama: Geor Davie ni mtumishi wa kweli