Na Aveline Kitomary, TimesMajira Online, Dar es Salaam
MCHUNGUZI wa dawa wa mamlaka ya dawa, vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) Gerald Sambu amesema ni muhimu kuangalia muda wa matumizi na usajili pale mtu anaponunua sanitizer ili kuweza kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
Akianisha madhara ya kutumia sanitizer isiyokuwa na Ubora leo jijini Dar es Salaam,Sambu amesema zinaweza kusababisha kuchanika kwa ngozi na kutokuangamiza vijidudu kama ilivyokusudiwa.
“Tukianza kupima sanitaizer tunapima kwanza kama kuna kiasi cha kilevi ‘alcohol’ inayotakiwa kwasababu sanitizer inapoandaliwa inatumika kemikali hivyo huenda kipimo cha tindikali na nyongo (PH) ikawa juu au chini ikaathiri ngozi.
“Kumbuka ngozi inapoathirika kwa kupaka sanitaizer inaweza kukusababisha maumivu mengine tunahakikisha usalama wa sanitizer kuhakikisha ubora wake.
Sambu amesema kiwango cha kilevi kinachotakiwa katika sanitizer ni 60 hadi 80 ili kuwa na ubora na ufanisi wa kufanya kazi vizuri.
“Ikiwa sanitizer ina alcohol nyingi labda 90 hadi 100 inasababisha ngozi kukauka haraka na kuchanika kwahiyo hata kama kuna bakteria au virusi anaweza asiuliwe vizuri hii inaweza kuleta maambukizi mengine hivyo tunapima tindikali na nyongo ili ngozi isiweze kuharibiwa”ameeleza.
Amesema pindi mtu anapopaka sanitizer mikononi inatakiwa kuchukua dakika moja kukauka
“Kitu cha kwanza unaponunua sanitizer hakikisha imesajiliwa pia ni muhimu kuangalia ‘expire date’ kuhakikisha ubora wa nje na unapochukua na kupaka haitakiwi kukukaa mkononi muda mrefu ikauke ndani ya dakika moja ukikuta unapaka inanata maana yake ina griseline nyingi haifanyi kazi yake vizuri na vijidudu havifi.
“Na pia endapo sanitizer itakauka ndani ya sekunde 10 inaweza isiwe na ufanisi katika mikono yako hivyo kiwango cha muda uliowekwa ndio sahihi,”amesema Sambu.
More Stories
Madaktari bingwa wa Samia watua Rukwa
Waliombaka, kulawiti binti wa Yombo, Dar jela maisha
Utashi wa Rais Samia na matokeo ya kujivunia vita dawa za kulevya nchini