December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Unawaji mikono ni njia madhubuti ya kuzuia maradhi ya maambukizi

Na Mohammed Sharksy,TimesMajira online

KUNAWA mikono kwa sabuni ni muhimu sana hasa katika mapambano dhidi ya maradhi ya kuambukiza hasa katika haya ya mifumo ya maradhi ya pumzi kama ugonjwa huu thakili wa COVID 19 ambao umekuwa ni janga kubwa sana duniani kote.

Unawaji wa mikono ni njia madhubuti ya kuzuiya maradhi mbalimbali ya kuambukiza. Ushahidi unaonyesha kwamba unawaji wa mikono wenye ufanisi huleta mafanikio makubwa sana ya kiafya katika jamii yoyote ile hapa duniani.

Tafiti zimeonyesha kwamba unawaji wa mikono kwa maji safi na salama yalioyotiririka na sabuni hupunguza vyanzo vikuu vya vifo vya watu wazima na watoto vitokanavyo na maradhi ya kuharisha na maambukizi ya mifumo ya kupumua kama vile corvid 19,homa ya mapafu, flu, chikungunya na kadhalika.

Kutokana na umuhimu wake Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na wadau mbalimbali walikaa nakujadili na kuweza kuanzisha siku maalumu ya kunawa mikono duniani ambao huazimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 15 lengo ni kuongeza juu ya uelewa kwa jamii juu ya maswala mazima ya umuhimu wa uanawaji mikono.

NINI MAANA YA KUNAWA MIKONO?

Kuna mikono ni utaratibu maalumu wa kuosha mikono kwa kutumia maji safi yenye kutiririka na sabuni kwa kufuata hatua maalumu kwa muda usiopungua sekunde 20.

Maradhi mengi yanayoikumba jamii zetu yanatoka na tabia ya kutonawa mikono ipasavyo, mfano wa maradhi hayo ni ni pamoja na maradhi ya kuharisha ikiwemo kipindupindu,kuharisha, damu, maraddhi ya minyoo, ugonjwa wa kope maradhi ya mifumo ya kupumuwa ikiwemo ugonjwa ulioikumba duniani kwa sasa ugonjwa wa Covid-19.

NI WAKATI GANI UNATAKIWA UNAWE MIKONO

Kabla na baada ya kushika au kula chakula chochote kinachohitajika kwa kwa kutumia mikono,baada ya kutoka chooni,baada ya kushika mnyama au kinyesi chochote kile ama cha binadamu au mnyama, baada ya kumsafisha mtoto aliyejiasaidia kwa njia kubwa au ndogo, kabla ya kutayarisha chakula, baada ya kushika taka taka zikiwemo zile za kufagia au kufanya shughuli yeyote ile ya usafi wa mazingira yetu yalio tukabili, baada ya kumudumia mgonjwa ,baada ya kukohoa au kupiga chafya na kadhalika.

HATUA GANI ZA KUCHUKUWA WAKATI UNANAWA MIKONO?

Ili kuhakikisha kwamba mikono yako iko safi na salama ni muhimu kupitia hatua hizi zifuatazo kwa ukamilifu iroweshe mikono yako kwa maji yenye kutiririka, Paka sabuni kuenea sehemu zote za mikono, hakikisha unadugua mikono mbele na nyuma, sugua kila kidole, kasha malizi kidole gumba pamoja na ncha za vidole ikiwemo kucha ili kuweza kuondoa uchafu wote uliojifisha ambao utakuwa vigumu kuufikia.

Mwisho unasuuza vizuri mikono yako kwa maji yenye kutiririka, kusha mikono ya yako kwa kitambaa safi, tishu, kwa kutumia mashine maalumu yenye ujoto kwa kukaushia au inua mikono yako juu kama ishara ya kushangilia.

JE KUNA FAIDA GANI ZA KUNAWA MIKONO?

Unaponawa mikono ipasavyo unaweza kujikinga na maradhi yafuatayo maradhi ya kuharisha, kuharisha damu,Ugonjwa wa Covid 19, Homa ya mapafu, Kipindupindu, ugonjwa minyoo, Ebola, Ugonjwa wa vikope, ugonjwa wa macho tongo, homa ya matumbo, homa ya mafua.

ANGALIZO

Ni muhimu sana kuepuka kunawa mikono ndani ya chombo kama kwenye ndoo, besen au sufuria nakadhalika daima nawa mikono kwa maji yenye kutiririka na epuka kutumia kitambaa cha mkononi au taula moja kwa watu wakati wa kukausha mikono.