Kwa kuwa kinara katika kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea kuhamasisha wananchi kutumia Nishati Safi ya Kupikia ili ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia nishati safi ya kupikia kama inavyoelekezwa katika Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034.
Hayo yameelezwa Mei 27,2025 katika Banda la REA Jijini Dar es Salaam na Mhandisi Miradi kutoka REA, Raya Majallah kwa Mkuu wa Mkuu wa Idara ya Nishati kutoka Umoja wa Ulaya, Max Pedetti.
“Tunaendelea na uhamasishaji wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia nyenzo mbalimbali ili kuhakikisha tunafanikiwa kufikisha lengo la asilimia 80,”amesema Raya.

Pedetti amepongeza jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na REA na alisisitiza REA iendelee na utoaji wa elimu ili wananchi watambue umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia.
Katika maadhimisho hayo REA kwa kushirikiana na wadau wake imepata fursa ya kuonesha teknolojia za bidhaa mbalimbali za nishati safi ya kupikia, sambamba na kushiriki kikamilifu mijadala mbalimbali kuhusu nafasi ya nishati jadidifu katika kufikia lengo la taifa la kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo 2034.
Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu yamefunguliwa rasmi na Mkuu wa Idara ya Nishati kutoka Umoja wa Ulaya, Max Pedetti akimwakilisha Balozi wa Umoja wa Ulaya.
More Stories
Prof.Mbede:Nishati ya umeme wa Sola imepunguza vifo vya wajawazito
Rais Samia apongezwa kuanzisha bima ya afya kwa wote
Serikali yajipanga kudhibiti matumizi yasiyo sahihi kuelekea uchaguzi mkuu