Na Yusuph Mussa, TimezMajira Online
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge ameutaka Umoja wa Mataifa (UN) uweke kipaumbele katika miundombonu ya kidigitali ambayo italinda mifumo dhidi ya mashambulizi na uhalifu wa mitandaoni
Mhandisi Ulenge amemwaga tena cheche hizo Machi 13, 2023 kwenye Kongamano la Umoja wa Mataifa katika Bunge la Dunia (IPU) linalofanyika nchini Bahrain wakati anajibu swali lililoulizwa na Umoja wa Mataifa kuwa, nini iwe ni kipaumbele wakati ujao kwenye Ulimwengu wa kidigitali?
Mhandisi Ulenge alijibu kwa kusema kwamba, wana sayansi wanasema vita vijavyo vinatajwa kuwa ni kati ya binadamu na teknolojia, na binadamu anataka kuitumia teknolojia kukua kiuchumi, lakini wakati huo huo, mashambulizi ya mtandaoni na uhalifu wa mitandaoni unamrudisha nyuma binadamu kukua kiuchumi.
“Wana sayansi wanasema vita vijavyo vinatajwa kuwa ni kati ya binadamu na teknolojia. Binadamu anataka kuitumia Teknolojia kukua kiuchumi wakati mashambulizi ya mtandaoni na uhalifu wa mitandaoni unamrudisha nyuma binadamu kukua kiuchumi.
“Hivyo Umoja wa Mataifa uweke kipaumbele katika miundombonu ya kidigitali ambayo italinda mifumo dhidi ya mashambulizi na uhalifu wa mitandaoni. Wanaofanya biashara ya kuuza savers za mitandao wanapaswa kujali ulindaji wa taarifa binafsi, na Tanzania imeshatunga Sheria ya ulindaji wa taarifa binafsi” alisema Mhandisi Ulenge
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini