Na Hadija Bagasha Tanga,TimesMajira Online
Rais wa shirikisho la wachi mbaji wa madini Tanzania John Wambura Bina amesema ukosefu wa umeme wa uhakika katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga unachangia uzalishaji duni wa madini hatua iliyotajwa kuchangia kuathiri hali ya kiuchumi ya wachimbaji wenye viwanda na mchango wa pato la Taifa sambamba na kuwataka wachimbaji wa madini kuacha tabia ya kutorosha madini.
Raisi wa shirikisho hilo ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea wachimbaji wa madini wenye viwanda katika katika wilaya ya Handeni na Tanga.
Rais huyo amesema amejionea changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini Mkoani Tanga ikiwemo suala la umeme katika migodi ya kati hususani eneo la Handeni kwani vipo viwanda vinavyotarajiwa kujenga huku vingine vikiwa tayari vimekamilika vikikabiliwa na changamoto ya umeme wa uhakika.
Aidha amesema ili Mkoa wa Tanga uweze kufunguka ni lazima pawepo na nishati ya umeme wa uhakika jambo ambalo wamelazimika kuiomba wizara ya nishati na madini kupitia waziri wa madini Dotto Biteko kupeleke umeme Handeni kwa manufaa ya wachimbaji kwani viwanda vinachangiwa kuleta kuongeza pato la Taifa kupitia kodi.
“Suala jingine kubwa nililoliona Tanga ni uelewa wa wachimbaji juu ya sheria ndogo ndogo za madini na mahusiano juu ya viwanda na wenye wachimbaji wadogo lakini mahusiano kati ya wakubwa na wale wa kati pia mfumo mzima wa biashara hauko wazi hivyo naomba na nimekwishatoa maelekezo kwenye vyama vyangu kwa kushirikiana na ofisi ya RMO kuhakikisha kabla ya kwenda kwenye mkutano wa tarhe 22 kukutana na Rais tuwe na mkutano wa kisekta hapa Tanga hususani kwenye bei elekezi,”amesisitiza Wambura.
Raisi wa Shirikisho la wachimbaji wa madini Tanzania anakemea suala la utoroshaji wa madini huku akizungumzia wenye viwanda kuwasaidia wachimbaji wadogo .
“Nimejaribu sana kukemea suala la utoroshaji wa madini ninaomba wachimbaji wa Tanga popote mlipo mhakikishe mnafuata sheria kanuni na taratibu za sheria kwani ndio kutawasaidia kuonekana katika kapu la seriakli kwenye GDP na sisi tunachangia chochote,”amebainisha Wambura.
Kwa upande wake mmoja wa wakezaji wa madini jijini Tanga kutoka kiwanda cha Tanga Minning company Rajesh Lakhuni amemshukuru Rais Samia kwa kuonyesha nia ya dhati ya kuwasapoti wawekezaji lengo likiwa ni kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa kupitia kiwanda chao wawemeza kutoa ajira kwa watanzania lengo likiwa kuifanya nchi izidi kuwa na watu wanaochangia maendeleo makubwa ya viwanda huku akimpongeza Rais Samia kwa kuweza kuondoa changamoto zilizokuwa zikiwakabili wawekezaji wengi nchini.
Madini yanayopatikana Tanga ni pamoja na madini ya ujenzi,madini ya viwanda,madini ya dhahabu,madini ya vito sambamba na madini ya chumvi.
More Stories
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake