Na George Mwigulu,Timesmajiraonline, Mpimbwe.
UKOSEFU wa maji katika baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi umetajwa kuwa chanzo cha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kushindwa kutumia vyoo vya kisasa mashuleni.
Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mustapher Kipeta amesema hayo Novemba 11, 2024 wakati wa baraza la madiwani ambapo ameeleza kushindwa kutumia vyoo ni chanzo cha wanafunzi kwenda kujisaidia vichakani.
Wanafunzi kwenda kujisaidia vichakani imekuwa rahisi kwao kwa sababu huko hakuna haja ya kutumia maji jambo ambalo ni hatari linaweza kusababisha magonjwa ya mlipoko kwa jamii.
“Changamoto kwenye kikao chetu leo ni maji, Ni kweli tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa jitihada ya miradi anayoileta lakini ukilinganisha na uhalisia tumezungumza bado kuna linkage, uharibifu na usimamizi mbovu na tumemwagiza Meneja wa RUWASA kwenda kuyasimamia” Amesisitiza Kipeta.
Ameongeza “ Kuna baadhi ya maeneo ukilinganisha na geografia yetu ya Mpimbwe bado yako maeneo makubwa ambayo yanashida ya maji na maji yanahitajika, kuna shule zimejengwa za kisasa zilizo na vyoo vya kutumia maji. Sasa maeneo hayo maji hayapo na kitongoji tu ili kuweza kupata maji wananchi wanakwenda umbali wa Km 10 hadi 15 ndipo wapate maji”
Kipate kutokana na changamoto hiyo ya maji anauliza je vyoo hivyo watavitumiaje?. Huku akisisitiza kuna uhitaji wa maji mkubwa na shida ya maji ni kubw, Na pale ambapo huduma ya maji imekwisha fika bado kunausimamizi wake ni mbovu.
Sambamba na hayo ameiomba serikali kuendelea kutenge fedha kwa ajili ya kupeleka miradi ya maji katika halmashauri hiyo ili kuweza kuondoa changamoto ambayo wananchi inawakabili kwa muda mrefu.
Diwani wa viti maalumu, Jenita Buswelu amesema kuwa wanafuzi ili waendane na mfumo wa matumizi ya vyoo vya kisasa maji yanahitajika nani lazima.
Jenita amesema kukosekana kwa maji inawaathiri wanafunzi na kuchukua uamuzi wa kwenda vichakani kujisaidia jambo ambalo si hatari kwa usalama wao pekee bali na jamii yote kwa ujumla.
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mlele, Yohana Marwa,amesema kuwa katika maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto ya maji tayari wameshatuma ombi la fedha Bilioni moja kwa ajili ya kutatua kero hiyo.
Meneja huyo ameweka wazi kuwa baada ya kupatikana kwa fedha hizo wataweza kusambaza mabomba kuanzia Mamba hadi Majimoto na kuoandoa mgao wa maji sambamba na kusambaza huduma ya maji kwenye maeneo mengine.
Marwa amesema serikali kupitia visima vya jimbo la Kavuu imejipanga kuchimba visima vitano kwenye maeneo mbalimbali ili kuhakikisha chagamoto ya maji inatoweka ndani ya halmashauri hiyo.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam