Na Esther Macha,timesmajira,online,Mbeya
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera ,Uratibu na Uwekezaji,Mwl.Doroth Mwaluko amesema ukosefu wa maadili katika jamii umekuwa chanzo cha wasichana wengi kujiingiza kwenye vitendo vya ngono zembe mapema.
Amesema hali hiyo inawafanya wasichana hao kukatisha masomo kwasababu ya kupata ujauzito.
Akizungumza hayo jana Ofisi za Kikundi cha huduma za majumbani (kihumbe)kilichopo katika kata ya Sinde mkoani Mbeya,wakati alipotembelea mradi wa Dreams unaowahusu wasichana waliopita kwenye mazingira magumu,ambao upo chini ya kikundi cha huduma za majumbani (Kihumbe)kwa kushirikiana na wadau mbali mbalimbali wakiwemo walter Reed na HJFMR.
Mwl.Mwaluko amesema kuwa wasichana wamepata nafasi ya kuunganishwa kupitia mradi wa Dreams na kupewa fursa mbalimbali ikiwemo ushonaji na ufundi magari hivyo hawana budi kutobweteka na badala yake waangalie fursa zingine ambazo zitaweza kuwakwamua kiuchumi.
“Ninachowasihi wasichana mmetolewa huko kwenye mazingira magumu na hatarishi,msirudi nyuma tena, wala msifanye mmebadilika mbele za watu kumbe mnaendelea kufanya mambo yenu kwa kificho hiyo haitapendeza lazima muwe mabalozi kwa mabinti wengine”amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi ,Dkt.Leonard Maboko amesema kila siku watu 200 nchini wanapata Maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi,huku asilimia 40 ya maambukizi hayo yakichangiwa na kundi la vijana.
Dkt.Maboko amefafanua takwimu hizo ni Sawa na vijana 80 wanapata maambukizi mapya kila siku, wengi wao wakiwa na umri kati ya miaka 15 hadi 24.
Amesema hali hiyo inatishia ustawi wa maendeleo ya nchi kwa kuwa kundi kubwa linaloathirika ni nguvu kazi ambayo inahitajika kusukumu gurudumu la maendeleo.
Balozi wa wasichana hao walio chini ya mradi wa Dreams, Joyce Masele amesema umekuwa mkombozi Kwa wasichana waliopita kwenye mazingira hatarishi ikiwemo kudhalilishwa kingono.
More Stories
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi
Rais Samia apongezwa kwa miongozo madhubuti ya ukusanyaji wa kodi
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru