Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
MKUU wa mkoa wa kilimanjaro Nurdin Babu amewakikishia wakazi wa Wilaya za Same na Mwanga kuwa tatizo la uhaba wa Maji litamalizika kabla ya Mwaka 2024 utakapokamilika Mradi mkubwa wa Maji Same, Mwanga-Korogwe.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya wilayani Same na kuwataka Madiwani wa Halmashauri hiyo kueneza taarifa hizo kwa Wananchi waweze kufahamu hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani.
“Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassani ametoa fedha nyingi kuakikisha Mradi huu Mkubwa wa Same Mwanga korogwe unakamika kwa wakati kuwawezesha wananchi kunufahika na Mradi huo”. amesema Mkuu wa Mkoa.
Aidha amesema, kazi kubwa ya Madiwani ni kumsaidia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani Katika utekelezaji wa Miradi na kuwaelimisha wananchi kufaham faida ya Miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Mbali na hayo Mkuu huyo wa Mkoa amewataka Madiwani kushirikiana kikamilifu katika kutoa Elimu kwa wananchi na pia kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani katika kuleta maendeleo.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba