Na Mohammed Sharkys,TimesMajira online
MAUMIVU ya viungo ni ugonjwa wa kusagika kwa viungo vya mifupa ambalo ni tatizo sugu linalowasumbua watu wengi katika jamii yetu kwa sasa kutokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha.
Umri mkubwa ni moja ya sababu inayopelekea kutokea kwa tatizo hili,ambapo tishu za mwili zinakuwa kavu.
Watu wengi wanafikiria kwamba kufanya mazoezi ni hatari kwa afya ya viungo lakini ukweli ni kwamba ili kuepuka magonjwa ya viungo mazoezi ni lazima katika kuongeza ufanisi wa viungo vya binadamu.
Ugonjwa wa kusagika kwa mifupa ya viungo ni ugonjwa unaotokana na hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha maumivu makali na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo.
CHANZO CHA KUSAGIKA KWA VIUNGO VYA MIFUPA (ARTHRITIS) NI NINI?
Ili kutambuwa chanzo cha ugonjwa huu, ni vizuri kwanza tutazame muundo wa viungo au sehemu mifupa miwili inapokutana.
Kwa mfano goti ambapo lina mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana,tishu za nyuzi zinazounganisha mifupa (Ligaments) ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja.
Hii ni kama utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje,ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.
Utando laini (Cartilage): Huu ni utando unaofunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja.Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita ngengedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.
Kifuniko/au utando ambao kazi yake inaupa ulinzi vile viungo (Capsule):Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu kuna umaji umaji (synovial fluid) ambayo huzalishwa na ute wa huo huo umaji umaji (Synovial membrane).
Synovial fluid ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane utando wa ndani wa viungo ambao inazalisha umaji umaji kazi yake kubwa ni kulainisha viungo lakini pia kazi nyingine inaipa chakula kwa ajili ya kurutubisha ngengedu kwa vile haina mishipa ya damu kupeleka chakula moja kwa moja ni utando ulio kwenye kuta za ndani za kifuniko.
DALILI ZA UGONJWA WA VIUNGO
Dalili kuu ya magonjwa haya ni maumivu makali na kukakamaa kwa maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.
Dalili zinaweza kuanza polepole au ghafla. Huu ni ugonjwa sugu na dalili zake zinaweza kuja na kuondoka,au kuendelea kuwepo kwa muda.
SABABU YA KUSAGIKA KWA VIUNGO
Ugonjwa wa viungo unasababishwa na hi! lafu yoyote ka! ka sehemu hizo za maungio ya mifupa.
Inaweza kuwa mifupa laini (ngegedu) kwa jina la kigeni linafahamika kwa cartilage inalika,Ngegedu kwa kawaida hulinda viungo na kuvifanya viwe laini ili vifanye kazi vizuri.
Aidha ngegedu pia husaidia kupunguza shinikizo kwenye viungo, kwa mfano,mtu anapotembea shinikizo kubwa huwa kwenye viungo vya miguu,ngegedu huisaidia mifupa kuhimili shinikizo hili.
Bila kiwango cha kawaida cha ngegedu au kama ngegedu imeharibika,mifupa husagana na kusababisha maumivu makali, kuvimba na kukakamaa kwa viungo.
Upungufu wa kilainisho cha mwili (synovial fluid),maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.
Ugonjwa huu husababishwa na kuharibika kwa ngegedu,kuvimba kwa viungo kunaweza kusababishwa na magonjwa yanayosababishwa na mfumo wa kinga (autoimmune) haya ni magonjwa yanayosababishwa na mfumo wa kinga kushambulia tishu za mwili kimakosa na kuziharibu.
Kwa kawaida,uvimbe wa viungo huondoka baada ya kutibiwa hata hivyo baadhi ya wakati uvimbe hauondoki.Hili linapotokea, una yabisi-kavu sugu,ambapo ugonjwa huu naweza kutokea kwa wanaume au wanawake lakini aina nyingi za ugonjwa huu huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume.
Asilimia 60 ya watu wenye yabisi-kavu ni wanawake.Na ile ya Jongo ‘gout’ inawapata zaidi wanaume kuliko wanawake.Yabisi inayotokana na kusagika viungio (Osteoarthritis) ndio aina ya yabisi- kavu inayowapata watu wengi zaidi.
WATAALAMU WANASEMAJE?
Akizungumza na makala haya,Hamidi Abdallah Massoud, Daktari bingwa wa magonjwa ya mifupa kutoka Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja alizitaja sababu ya umri inachangia sana ugonjwa huo.
Anasema kila umri unapoongezeka hatari ya kupata ugonjwa ni mara mbili zaidi,Sambamba na kuchangiwa na uzito mkubwa, majeraha na kuumia kwenye viungo navyo huchangia sana ugonjwa huu.
Nae daktari bingwa wa magonjwa ya mifupa,Shaibu Yussuf,anasema kuna baadhi ya kazi zinaweza kusababisha kupata ugonjwa wa kusagika kwa viungo hasa pale wakati wa kuchuchumaa au kupiga magoti.
AINA ZA UGONJWA WA VIUNGO
Ziko aina nyingi sana za ugonjwa wa viungo. Katika makala ya leo tutazungumzia aina nne ambazo ni maarufu na zinazowapata watu wengi.
Aina ya mwanzo ni ‘Juvenile rheumatoid arthritis’ni ugonjwa wa viungo ambao huwapata zaidi vijana walio chini ya umri wa miaka 18 na unakuja kwa namna nyingi.
Ugonjwa wa aina hiyo umegawika sehemu tatu ikiwa ni pamoja na Pauciarticular JRA,huu ndiyo unaoonekana zaidi na hauna madhara makubwa ukilinganisha na aina nyingine.
Mtoto atasikia maumivu kwenye viungo zaidi ya vitatu.Aina ya pili ni Polyarticular JRA,huu hushambulia viungo vingi zaidi ya vinne na maumivu yake huwa makali sana.
Systemic JRA, ugonjwa wa viungo huonekana kwa nadra ambapo maumivu hujitokeza kwenye maeneo mengi na madhara yake kuwa makubwa zaidi.
Mara nyingi mtoto huaanza kusikia homa za vipindi ambapo huzidi zaidi nyakati za jioni.Hali hii inaweza kumtokea mtoto kwa muda mfupi au kwa wengine kwa muda mrefu sana.
Mtoto atapata mauvimu kwenye maungio ya mifupa, uvimbe kwenye maungio hayo na kukakamaa kwa viungo.Mtoto huyu kukosa hamu ya kula na hivyo kumfanya akon
njwa ukizidi,mtoto anaweza kudumaa (kushindwa kukua), ukuaji wa mifupa yake kuathirika na kupata matatizo ya macho (uveiti).Osteoarthritis: Ugonjwa wa viungo unaowasumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine yoyote ugonjwa huu unawapata zaidi wazee (watu wenye umri mkubwa).
Osteoarthritis hutokea pale mifupa laini inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka.Mifupa laini ni viungo vinavyohimili migandamizo ya ghafl a (shocko absorber).
Mifupa laini hii huwa inapopoteza ubora wake,tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu makali.Hali hii ya uharibifu huu wa mifupa laini ikiendelea,mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana.
Athari za ugonjwa huu huanza taratibu na kuongezeka na hutokea maumivu kwenye viungo hasa baada ya kufanya shughuli fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu.
Viungo huwa vinakaza sana mapema asubuhi pale mtu anapotaka kuanza shughuli za kawaida.Rheumatoid arthritis: Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili kwa bahati mbaya kuanza kushambulia viungo vya mwili ikiwa ni pamoja na synovial membrane na kusababisha uvimbe na maumivu.
Hali hii isipodhibitiwa,huweza kusababisha ulemavu,ambapo ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho,ngozi, mapafu, midomo,damu na mishipa ya damu.
Huu ni ugonjwa ambao zaidi ni wa wanawake na huwatokea zaidi wawapo kati ya umri wa miaka 40 hadi 60.
Mgonjwa atasikia maumivu na kuona uvimbe kwenye viungo vya pande zote za mwili,mfano magoti yote mawili vidole, viwiko vya mikono na miguu.
Athari zake huonekana zaidi asubuhi unapoamka na maumivu yanaweza kudumu kwa muda wa hadi nusu saa. Muathirika wa ugonjwa huu hujisikia mchovu muda wote, hukosa hamu ya kula na hupungua uzito.
MATIBABU YAKE
Matibabu ya ugonjwa wa kusagika kwa viungo ni hali ya kudhibiti maumivu yasiendelee,kupunguza uharibifu wa viungo na kuboresha au kudumisha kazi ya viungo kwa mfumo bora wa maisha.
Kulingana na madaktari,matibabu ya ugonjwa wa kusagika kwa viungo huhusisha dawa za maumivu na kupunguza uvimbe,tiba ya mazoezi ya viungo au tiba ya kazi,kupunguza uzito na upasuaji pale inapobidi.
More Stories
Boost ilivyoboresha miundombinu ya elimu IlemelaÂ
Samia apongeza walimu 5,000 kupatiwa mitungi ya gesi, majiko kutoka Oryx
Uwekezaji kwenye kilimo utatimiza ndoto ya Samia ya nchi kuwa ghala la chakula Afrika