May 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ufaransa yatoa shilingi Bilioni 1.6 Kwa vikundi vya singeli

Na David John timesmajira online 

SERIKALI ya ufaransa kupitia ubalozi wake hapa nchini imetoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 Kwa wasanii mbalimbali wakiweno wa mziki wa Singeli,Sanaa, pamoja na eneo la uchapishaji wa vutabu  hasa kidigitali na fedha hizo zinakwenda Moja mwa Moja mwa Taasisi hizo.

Akizungumza  mbele ya katibu mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na michezo   Said Yakubu  mapema wiki hii Balozi wa ufaransa hapa nchini Nabil Hajlaoui Amesema kuwa nchi ya ufaransa Kwa kutambua mahusiano yake na Tanzania itaendelea kusaidia makundi mbalimbali ikiwamo mziki wa Singeli  kwa lengo la kuutambulisho mziki huo  Duniani.

Amesema kuwa kupitia kituo cha Utamaduni cha Alliance Francie  Serikali ya ufaransa imetoa fedha hizo kiasi cha sh.bilioni 1.6 Kwa ajili ya maeneo hayo na maeneo mengine Ikiwa pamoja kuunga mkono katika kile ambacho wasanii hao wanakifanya.

“kiasi hiki cha fedha naamini kinatakwenda kuusogeza mziki wa Singeli na kuutambulisha  Duniani kama kauli mbiu inavyosema kuwa “Singeli twende zetu 2 the world” na Serikali itaendelea kusapoti vikundi mbali mbali na hii nikutokana na mahusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi mbili.”Amesema Nabil Hajlaoui

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Sanaa ,michezo na Utamaduni yakubu anashukuru  Serikali ya ufaransa Kwa kutoa fedha hizo ambazo zinakwenda kwenye maeneo hayo na fedha hizo zitakwenda kusaidia kuuza mziki wa Singeli nje ya Tanzania kupitia mradi wa Singeli 2 the world lakini pia upo mradi mungine ambao unafadhiriwa ambao ni wakugundua vipaji vya Singeli katika mikoa ya Tanga,Dar es Salaam ,Morogoro.

Amesema kuwa mradi huo utajimuisha mabiti vijana Kwa ajili ya Kuitangaza mziki wa Singeli na vile vile zinakwenda kutengeneza mradi wa kigitali wa vitabu kupitia kampuni ya    mkuki na nyota ,kundi la melaki Kwa ajili ya maonyesho ya mavazi Kwa miradi ambayo wanayo na melaki ni mkusanyiko wa wasanii kadhaa katika sekta hiyo.

“Kwaujumla sisi kama Serikali tunashukuru sana ubalozi wa Ufaransa Kwa maana Serikali ya nchi hiyo kupitia Kwa Balozi wake Nabil Kwa msaada huu na sekta zetu kama mnavyofahamu nisekta ambazo zimejaa ubunifu, lakini kinachokosekana ni suala la uwezeshwaji wa mitaji ya kuweza kufikia ndoto na zikaweza kufikia hivyo msaada kutoka Kwa mdau yeyote tunapokea Kwa mikono miwili na tumeawaasa wanaosaidiwa fedha waifanye tanzania ijivunie wao ili misaada mingine iweze kutiririka zaidi Kwa kusaidia.”Amesema 

Nakuongeza kuwa “mnafahamu kuwa Rais Dkt Samia Hassan Suluhu alikwishatoa shilingi Bilioni 2.5 kusaidia wasanii kupitia mfuko wa wasanii na fedha hiii kutoka ufaransa na yenyewe ni katika maono hayo hayo ya mh Rais Dkt Samia.”amesisitiza katibu Yakubu

Kwaupande wake Abas Ally Jaza ambaye ni Meneja wa Singeli Amesema Imani yake nikuona fedha hizo zinakwenda kuzalisha wasanii wengine wapya ambao wamekosa nafasi huku wakilenga zaidi watoto wakike kwani wanawake kwenye mziki wa Singeli wamekuwa sio wengi sana na wanaopata nafasi ni wachache sana hivyo watajaribu kuchukua wasanii watakaopendekezwa na wataalumu wengine .

Pia baada ya kuwapata wasanii hao watakaa nao kwenye nyumba ya Singeli Kwa mwaka mmoja Kwa ajili ya kuufundisha kupata mziki mzuri na mwimbaji anavyofakiwa kuwa na kuweza kuimba vizuri.