Na Aveline Kitomary,TimesMajira Online ,Dar es Salaam
DHANA ya neno ‘diet’ kama inavyotafiriswa na baadhi ya watu huenda ikaweza kuwasababishia matatizo hasa ya macho kutokana na ulaji wa vyakula visivyo na virutubisho ya kutosha vinavyohitajika mwilini.
DAKTARI Bingwa wa Macho kutoka hospitali ya Macho (CCBTR) Dk Cyprian Ntomoka anasema ufahamu mdogo kuhusu mlo kamili (balance diet) unaweza pia kuwa chanzo cha matatizo ya macho katika jamii.
katika mahojiano maalum na Jarida la Majira ya Afya anasema kuwa watu wamekuwa na mtindo wa kula aina Fulani ya chakula au kujinyima kula wakiita ‘diet’ huku wakiwa hawana uelewa wa kutosha katika kuhakikisha wanapata virutubisho vinavyohitajika katika mwili.
Dk Ntomoka anasema watu walisiokula vyakula yenye vitamin wala madini wako katika hatari ya kupunguza kiwango cha kuona au kutokuona kabisa.
Anashauri watu kuzingatia ulaji wa vyakula vyenye zink maziwa ya ngo’mbe,mboga za majani ,nafaka isoyokobolewa ili kuboresha zaidia afya ya macho.
“ Lishe inaweza kuathiri uwezo wa kuona si mara chache utakutana na mtu ambaye ameambiwa avae mewani akaitupa na kwasababu ameambiwa ale karoti ,mboga za majani hivi ni miongoni mwa vyakula ambavyo vinasaidia.
“Kila sehemu ya jicho inaaina ya kirutubisho ambacho kinaweza kufanya jicho kufanya vizuri zaidi ,sehemu ya mbele ya jicho (cornea) inakusanya mwanga na kupeleka katikati ili mtu aweze kuona inauteute ambao unalaisha sehemu hiyo na kunavyakula ambavyo vinasaidia kama vyakula vya vitamin A, mboga za majani ,mbogamboga inasaidia jicho kuona vizuri,”anasema.
Dk Ntomoka anasema kwa kipindi cha nyuma mtu akiwa na tatizo la utapiamlo anapata kovu mbele ya jicho kwasababu zile seli pale zikipungukiwa na vitamin A zinashindwa kufanya kazi vizuri na kutengeneza kovu.
“ Na matibabu yake ni matone ya vitamin A ndo maana hata watoto wanapozaliwa wanapewa matone hayo ili kusaidia kutengeneza sehemu ya mbele ya jicho iweze kufanya kazi vizuri.
“Kwahiyo mtu anayekula mboga za majani na kuwekewa karoti anasaidia sehemu ya mbele ya jicho kufanya kazi vizuri.
“Kwahiyo mtu ambaye hana vitamin A nikimaanisha hali mboga za majini na mbogamboga seli zikifa hazihuishwi kwa haraka na isipohuishwa mtu naweza kupata shida ya kuona usiku(night blindness),”anabainisha.
Anasema ukosefu wa virutubisho muhimu vinavyohitajika pia huweza kuathiri mshipa wa fahamu katika jicho.
“Tafiti zinaonesha kuwa kuna vitamin B12, B6, na B3 zinasababisha mishipa ya fahamu kuweza kufanya kazi vizuri ,mishipa ya fahamu ndio mbayo inachukua picha kwenye ubongo.
“ Vyakula ambavyo vinautajiri sana wa hivi vitamin ni mazao ya nafaka isiyokobolewa Mfano mahindi ugali wa dona ni mzuri zaidi lile ganda limejaa hizo vitamin na aina ya madini ya zinc zinafanya kwa pamoja kuhakikisha mshipa wa fahamu unapeleka taarifa kwa ubongo,”anaeleza.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato