Na David John,TimesMajira,Online
SERIKALI ya Ufaransa kupitia ubalozi wake nchini Tanzania imewashindanisha wajasiriamali 1,000 kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania.
Ambapo washindi wa shindano hilo la wajasiriamali wamepata zawadi mbalimbali hii ikiwa ni kuwatia moyo katika shughuli zao za kijasiriamali.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa wajasiriamali hao,Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frédéric Clavier amesema vyombo vya umma na binafsi kuendelea kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha malengo makuu yaliyoorodheshwa katika mpango mkakati wa “Tanzania 2025”.
“Ni bahati yangu kuwakaribisha kwenye sherehe ya kuwapongeza washindi wa shindano la Wajasiriamali 1000 ambayo Ufaransa tumeandaa, hafla yetu ya “kiuchumi na biashara” iliyowekwa katika Mkutano wa “2020 Africa France Mkutano,”amesema na kuongeza kuwa
“Naomba kusisitiza kiwango cha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa na kati ya Ufaransa na Tanzania tutaendelea kukiimarisha,”amesema
Ameongeza kuwa sekta ya umma ikiwa ipo mstari wa mbele kuleta uchumi kwa kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ni vizuri sekta binafsi nayo ipate nafasi ya kushiriki kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kupendekeza ubunifu na suluhisho endelevu.
More Stories
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang
Daktari Dar ajishindia Mil. 100/- za Fainali NMB Bonge la Mpango