Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katika jitihada za kutangaza na kubidhaisha lugha ya Kiswahili, Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kwa kushirikiana na Mamlaka ya mji wa Enzikreis, Ujerumani tarehe 07/07/2024, ulifanya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani.
Maadhimisho hayo yaliambatana na burudani mbalimbali ikiwemo nyimbo za Kiswahili na muziki wa Kiswahili. Washiriki pia waliweza kula vyakula vya kitamaduni vya Kiswahili.
Aidha, Mheshimiwa Balozi Hassani Iddi Mwamweta kwa niamba ya Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), aliwakabidhi vyeti vya utanbuzi walimu mbali mbali wa Kiswahili pamoja na kutoa vitabu vya kiada na ziada kwa wanafunzi wa lugha ya Kiswahili kwa lengo la kuwawezesha kujifunza lugha ya Kiswahili kwa ufanisi zaidi.
Kutokana na hamasa inayotolewa kuhusu lugha ya Kiswahili, kumekuwa na ongezeko la raia wa Ujerumani wanaojifunza lugha ya Kiswahili.
More Stories
Kapinga asema mafanikio katika sekta ya nishati yanatokana na jitihada za Rais Samia
Bumbuli kutekeleza miradi kwa kuangalia vipaumbele
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi