December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

U.S CDC na Amref Health Africa Tanzania kusaidia Serikali Kukomesha janga la UKIMWI ifikapo mwaka 2030 Mkoani Mara

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Shirika la Amref Tanzania kwa msaada wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) kupitia Vituo vya Kudhibiti Magonjwa vya Marekani (CDC) nchini Tanzania, inafuraha kutangaza upanuzi wa afua inayoendelea ya afya inayoitwa ‘Afya Kamilifu Project’ mkoani Mara.

Mradi wa Afya Kamilifu ni mpango wa miaka mitano wa dola 50,000,000 unaotekelezwa hivi sasa huko Tanga, Zanzibar, Simiyu na sasa mkoani Mara kwa lengo la kuongeza juhudi za matunzo na matibabu ya VVU, ikiungana na juhudi za kimataifa za kukomesha janga la UKIMWI ifikapo 2030.

Kwa kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa katika Mkoa wa Mara, CDC, Amref Tanzania na washirika wengine wa utekelezaji; Chuo Kikuu cha Maryland- Baltimore na Kituo cha Mawasiliano na Maendeleo Tanzania vitashirikiana kudhibiti janga la VVU.

Mipango itajumuisha hatua zinazolengwa kufikia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na kuwaweka kwenye matibabu; utambuzi wa mapema na matibabu ya kifua kikuu (TB), upimaji wa kina wa VVU, na kupanua wigo wa dawa za VVU na TB, na kuzuia na kudhibiti maambukizi.

Malengo ya Mradi wa Afya Kamilifu yamejengwa juu ya PEPFAR na Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu VVU/UKIMWI malengo ya kasi ya 95-95-95 ifikapo mwaka 2030. 

Mfumo wa 95-95-95 unamaanisha kuwa ifikapo 2030, 95% ya watu wanaoishi na VVU. VVU wanajua hali yao ya VVU, wakati 95% ya watu wanaojua hali yao wanatumia matibabu ya kudumu ya kurefusha maisha, na 95% ya watu wanaopata matibabu hupata ukandamizaji unaohitajika wa virusi.

Uzinduzi wa Mradi wa Afya Kamilifu mkoani Mara ulifanywa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma  Dk Khalfan Haule ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe Ally Happy.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau kadhaa, wakiwemo maafisa wa serikali ya Tanzania, mwakilishi wa CDC Tanzania, Usimamizi na Wafanyakazi wa Amref Health Africa Tanzania, mashirika ya kiraia, washirika wa utekelezaji, vyombo vya habari, washirika wa maendeleo, viongozi wa Dini wa Kanda na sekta ya kibinafsi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Khalfan Mkuu wa Wilaya ya Mara alipongeza juhudi za shirika la Amref’s na washirika alitambua katika utekelezaji wa Mradi wa Afya Kamilifu Mkoani Mara.

“Kuwa na mradi huu ni hatua nzuri katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI nchini, tunaishukuru Wizara ya Afya ambao wako kwenye kiti cha udereva katika mpango huu, tunashukuru kwa vitendea kazi vilivyotolewa na CDC na AMREF ambavyo vitasaidia.” Amesema Dkt. Khalfan

Mwakilishi wa CDC, Dk. Eva Matiko, amesema muwa vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Marekani, vinathamini ushirikiano na juhudi za mpango wa Amref’s Afya Kamilifu kusaidia programu huko Mara, Tanga, Simiyu na Zanzibar.

“Tunathamini fursa ya kushirikiana na Wizara ya Afya, viongozi wa mikoa, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha matokeo ya afya nchini Tanzania”.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk.Florence Temu, mradi huu unalenga kuongeza idadi ya watu wanaoishi na VVU na UKIMWI wanaojua hali zao kupitia upimaji wa VVU na kupata huduma za muda mrefu na endelevu za dawa za kurefusha maisha (ART).na upimaji wa Mzigo wa Virusi ili kuhakikisha kuwa wanapata ukandamizaji wa virusi wa kiwango kisichoonekana. “Mwisho wa mradi tunatarajia watu wote wanaoishi na VVU mkoani Mara wajue hali zao na kupata matibabu.

Mradi pia utaimarisha mifumo ya kuwaunganisha watu walioambukizwa VVU na huduma za matunzo na matibabu na kuhakikisha uwepo wa mifumo ya maabara inayofanya kazi vizuri na kusaidia huduma za kliniki za VVU katika vituo vyote vya afya” alifafanua.

“Mradi pia utaanzisha mfumo thabiti wa ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za VVU katika wakati halisi kwa kutumia teknolojia ya kibunifu ambayo itahakikisha upatikanaji wa haraka wa data sahihi na bora kutoka ngazi ya kituo hadi ya kitaifa kwa ajili ya kufanya maamuzi na kuripoti kimataifa.

Inatarajiwa kwamba ripoti hizi za ubora wa data zitatumika kusaidia mifumo ya usimamizi wa data katika ngazi ya kituo na kujenga uwezo wa umiliki wa data na kuboresha usimamizi na matumizi ya data katika vituo vya kutolea huduma za afya na Timu za Usimamizi wa Afya za Wilaya ili kubaini mapungufu katika utoaji wa huduma za VVU na kuboresha ipasavyo” aliongeza.

‘Afya Kamilifu’ Mradi ni mojawapo ya mipango ya afya ya Amref nchini Tanzania, ambayo itachangia kupunguza mzigo mkubwa wa VVU na UKIMWI nchini, ambapo zaidi ya Watu Milioni 1.4 Wanaoishi na VVU ambayo ni asilimia 5 ya Watanzania wa miaka 15-64. Kwa mujibu wa Utafiti wa Athari za VVU Tanzania (HIS) 2016-17. Zaidi ya hayo, utafiti unaonyesha kuwa kiwango cha ukandamizaji wa wingi wa virusi miongoni mwa rika moja nchini Tanzania ni 87.0%.